Find us on facebook

Pages

Follow Me.

Saturday, October 26, 2013

HABARI KUHUSU MBOWE KUMILIKI MAJUMBA ZACHUKUA SURA MPYA:

By Haki sawa View Post
Kutokana na mjadala ambao tayari umeshawekwa hapa na kujadiliwa kwa siku mbili mfululizo , nimeona kuwa kuna watu wanafanya propaganda badala ya kujaribu kuutafuta ukweli wa jambo lenyewe na kuangalia rationale ya jambo linalojadiliwa .
Mimi niliamua kufanya jambo moja la kujaribu kuangalia nini alichokua amedeclare Mbowe kwenye Tume ya maadili ya viongozi kwa mujibu wa Sheria ya maadili ya viongozi wa umma , nimekuwa mambo yafuatayo na kama yupo ambaye anaweza kunichallenge na aje a seem hapa na sio kuhangaika na Gutter politics ,

Mbowe Freeman , kwenye fomu zake alideclare kuwa anamiliki nyumba kwenye nchi

JK: CCM INAWEZA KUNG'OKA 2015

Dodoma. Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Kikwete amesema kama rushwa haitakomeshwa ndani ya chama hicho, katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwaka 2015 kitaanguka vibaya na iwapo kitanusurika hakitapita kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.Katika hatua nyingine, Rais Kikwete

ICC,"RUTO SHARTI ASHIRIKI KESI YOTE"

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC imeamua sharti Naibu Rais wa Kenya William Ruto avihudhurie vikao vyote wakati wa kesi yake ambapo ameshtakiwa kutekeleza uhalifu wa kivita. Viongozi wa mashtaka walipinga uwamuzi wa awali ambapo Bw Ruto angekubaliwa kushiriki vikao vichache tu huku akitumia muda wake mwingi nchini Kenya.
Hata hivyo mahakama imesema licha ya uwamuzi huo

Monday, October 14, 2013

KATIKA HILI NANI WA KULAUMIWA?

                   Nawasalimia waungwana wote.Leo ndio siku alipofariiki muasisi wa taifa hili Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.Tanzania inasemekana ni nchi inayoendelea.Ukweli wa hili wnaujua wale wanaokaa katika nchi yeneyewe.kiujumla nchi inayoendele hadi watu wake watakuwa wanaendelea pia.Tunatatarajia kuona mabadiriko kulingana na maliasili tuliyonayo na si chini ya hapo basi kama tuna maliasili chache na mababdiriko yatakuwa ya ile malisaili chache.Baba katika familia anaendele kulingana na kazi na mtaji anaoutumia katika kufanya maendeleo yake.Ikiwa baba ana kazi nzuri na hata nyumba hana basi familia itajua huyu baba wa hapa atakuwa ni mfujaji wa kipato cha familia.Hivo basi wataamini kwamba anaelekeza pesa katika sehemu kusiko takiwa.Hivo basi Nchi hii imekuwa ni kama familia iliyotelekezwa na baba na ikabaki na mama mwenye upendo ila hana uwezo wa kutunza hiyo familia.Na cha kusikitisha zaidi hata watoto ndani ya familia hawawezi kumsaidia mama akapata kipato na kuendeleza familia ile.Tanzania imekuwa ni nchi ya mtu mle mtu.
           Wananchi wa hali ya chini wamekuwa wakiisha kwa hali ya vita vya weneyewe kwa wenyewe kwa wenyewe na nafsi zao.Wanapigana vita na nafsi zao huku wakiwaza nini watakachokula leo huku wao wakiwa ndio watendaji wakuu na kulipa kodi ambazo zimeendelea kuwaneemesha wakubwa.
           Wananchi matatizo waliyonayo ni suala zima la umasikini ambao umewafanya wawe ni watu wakufikiria suala zima la kutafuta ela ya kula tu mchana na usiku na sikufanya shuguli nyingine.Hao hao wanofanya biashara ndogo ya kuwalisha watoto wao hao hao ndio wanaodaiwa kodi kwa kupigwa virungu na Mgambo huku kodi yao ikienda kuliwa na watu bila kuwasaidia hao walipa kodi anagalau kuwajengea vibanda wafanyie biashara yao bila kupigwa na jua.Hao hao ndio wanaojengewa visima vya maji na serikali kwa gharama ya kodi yao na hapo hapo kulipia maji walioyajenga wao na hutoka kwemye ardhi waliyotunukiwa na mola wao.Watanzania licha ya kudhurumiwa haki zao wamekuwa pia wakinyamazishwa wasidai haki zao zilizodhurumiwa.Ama kweli SIJUI NANI ALAUMIWE?
            Licha ya kuishi katika mazingira magumu ya namna hii.Wapo wale amabao tiyari w aalishafanya raia wa hali ya chini kama misukule.MISUKULE hulimishwa kila siku usiku kucha na msukule wakati huo msukule huambulia chakula aina ya UNGA bila hata kusongwa.Wakati wale wanomiliki misukule hufurahia kwa kucheza ngoma na kufurahia mavuno yaliyolimwa na misukule hao.Mwisho wa siku misukule hao hukatwa ulimi ili asiweze kuongea kipi kinachoendelea kati yake na yule aliyemfanya msukule.Hatimae huyo msukule atakufa na kuliwa nyama na mwenye msukule huyo.
Watanzania chonde

Sunday, October 13, 2013

MWANDISHI WA HABARI UFOO SARO WA ITV NA RADIO ONE APIGWA RISASI PAMOJA NA MAMA YAKE.

Taarifa za mwanzo za kusikitisha ambazo tumezipata hivi punde zinasema mtu mmoja anayedhaniwa kuwa mume au mchumba wa mwandishi wa habari wa ITV na Radio One Ufoo Saro amefanya mauaji ya kutisha na

Saturday, October 12, 2013

YAONE MAGARI ALIOYOTUMIA MWL JULIUS KAMBARAGE NYERERE.

Gervas Mwatebela, Dar es Salaam 
Wasomaji wetu leo tumeamua kuangazia suala dogo tu katika utalii wa ndani kwa kutazama baadhi ya  magari aliyotumia Baba wa Taifa na Rais wa kwanza wa Tanzania Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wakati wa harakati za Uhuru na baada ya Uhuru mpaka alipofariki Oktoba 14,1999. Maelezo ya makala haya ni kwa mujibu wa nyaraka zilizopo Makumbusho ya Taifa, Dar es Salaam hasa kuhusiana na magari na miaka ya magari yalipotumika. Fuatana nasi.
1.AUSTIN MORRIS A-40
Gari aina ya  Austin Morris A-40 lilitengenezwa nchini Uingereza kati ya mwaka 1940 – 1950. Ni gari la kwanza kutumiwa na