Find us on facebook

Pages

Follow Me.

Wednesday, May 29, 2013

LADY JAYDEE, IZZO B,MWANA FA WAAHIRISHA SHOO ZAO KUMUENZI MANGWEA.

Baadhi ya wasanii wa bongo fleva nchini wameahirisha shoo zao kulingana na kile kinachotajwa na wao kwamba
ni kuonyesha heshima kwa msanii huyo.Baadhi ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya ni pamoja na Mwana Fa, Izzo  Business, pamoja na Kara Pina wamehairisha shoo zao ambazo zilikuwa zinatarajia kufanyika Mei 31 mwaka huu kwa sababu ya kifo cha msanii mwenzao Albert Mangwea kilichotokea jana nchini Afrika ya Kusini.

Mwana Fa ambaye alitarajia kufanya onyesho lake alilolipa jina la The Finest mwishoni mwa wiki hii amejikuta akiahirisha shoo hiyo kwa sababu ya msiba wa msanii mwenzao

Kwa upande wake Izzo Business alieleza  sababu ya kuahirisha shoo hiyo, alisema kuwa hawezi kuendelea na ratiba ya shoo hiyo wakati yupo katika wakati wa majonzi kwa kumpoteza msanii wao ambaye pia ni rafiki yao mpendwa .Pia msanii Jide NAYE ameahirisha shoo yake iliyokuwa ikitazamiwa kupigwa mei 31 na zitatajwa hapo badae.

No comments:

Post a Comment