Find us on facebook

Pages

Follow Me.

Thursday, May 23, 2013

MTWARA BADO HALI MBAYA MWANAFUNZI APIGWA RISASI.MAMA AUAWA.

Katika hali isiyo ya kawaida mjini mtwara eneo la Magomeni duru za habari zinzharifu kuwa.
Mwanafunzi  amepigwa risasi na mama mmoja amefariki dunia.
hivi sasa baadhi ya wananchi wa eneo la magomeni mkoani mtwara wamekimbilia katika Hospitali ya Mkoa wa Mtwara Lugula wakihofia usalama waokutokana na vurugu za kuchomwa kwa nyumba zao pamoja na vibanda vya biashara zilizotokea leo asubuhi katika eneo hilo.Maduka maeneo ya Magomeni yamechomwa moto ikiwamo pia mali za Askari magereza . Mwanafunzi wa CHUNO amefikishwa hospitali Ligula na majeraha ya risasi mguuni.  
Mwanamke mwingine anayekadiriwa kuwa na miaka 25 mjamzito ameuawa kwa kupigwa risasi maiti ipo LIGULA.Kwa sasa ( jioni  hii) inaelezwa kuwa katika baadhi ya mitaa hali imetulia na ni idadi ndogo ya wananchi ndiyo inayoonekana wakitembea mitaani isipokua eneo la magomeni ambako mbomu yanaendelea kusikika huku huduma za kijamii katika mji huo zikiwa zimesimama zikiwemo usafiri, huduma za kibenki na shule

No comments:

Post a Comment