Find us on facebook

Pages

Follow Me.

Monday, June 24, 2013

BAADA YA POLISI KUMKAMATA KADA WA CHADEMA MKEWE AANDAMANA.

MKE wa Kada wa Chama Cha Maendeleo na Demokrasia (Chadema) Joyce Kiria leo amejikuta katika wakati mgumu, baada ya kujitokeza mbele ya vyombo vya habari akiwa na watoto wake wawili wadogo,huku akimwaga machozi kutokana na kile alicho elezwa kwamba anamtafuta mumewake.
Mwanadada huyo ambaye ni mwanaharakati na mtetezi wa haki za wanawake amekuwa mhanga wa kazi yake ya utetezi wa wanawake baada ya Jeshi la Polisi nchini Tanzania kumficha mumwewe Henry Kileo.
Akizungumza na Habarimpya.com jijini Dar es Salaam, Kiria ambaye ni Mtangazaji wa kipindi cha Wanawake LIVE,kinachorushwa katika kituo cha Televisheni ya Chanel 5 (EATV) pamoja na DSTV, alisema kwamba mumewe ambaye ni kada wa Chadema aliitwa Polisi tangu siku ya Ijumaa iliyopita na kuwekwa rumande, lakini walipofuatilia tukio hilo wakaambiwa kwamba hajulikane alipo.
"Mume wangu aliitwa na jeshi la polisi tangu siku ya Ijumaa ya wiki iliyopita na alipofika kituo hapo aliamuriwa azime simu yake na kuwekwa kizuizini,tangu siku hiyo sijamuona mume wangu na sijui alipo, nikipiga simu yake haipatikani tulipokwenda Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam nikaambiwa kwamba hayupo kituoni hapo na hajulikani alipo"alisema Kiria na kuongeza huku akibubujika machozi:.
 
Leo tena nimekwenda kituoni hapo nikapewa jibu lisiloeleweka, kwamba Mumwe wangu alikuwepo hapo asubuhi lakini ameondolewa na kwamba haijulikani alipopelekwa, huku mtoa taarifa akidai kwamba pengine amepelekwa Tabora, sasa mimi nishike lipi ndugu zandu sijui mume wangu alipo na ameniacha na watoto wadogo kama mnavyo waona hapa".
Kiria alimtaka Rais Jakaya Kikwete pamoja na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Said Mwema kumweleza mumewe alipo, kwa sababu wasaidizi wao wameshindwa kuweka wazi alipo baba watoto wake.
"Haina haja ya wao kunificha alipo mume wangu, hata kama wamesha muua waniambie ilipo maiti yake, ili nikamchukue na kumzika na kama yuko hai waniambie alipo ili nimpelekee hata maji ya kunywa,sipingani na sheria pengine amefanya kosa kweli, lakini kila mtuhumiwa ana haki ya kuwasiliana na familia yake, kwanini wanampa mumewangu mateso makali kama hayo".Kaniacha na watoto wadogo Linkon (miezi 4) na Liston (miaka 2) mimi hawa watoto nitawapa nini katika maisha yangu, kama baba yao bado yuko hai waniruhusu nimuone, ili angalau anishauri jinsi ya kuwalea watoto wake"aliongeza Kiria.
Kiria ambaye aliandamana na ndugu zake wengine wanaoishi nyumbani kwake wakiwa na mabango yaliyokuwa ujumbe wa kutafuta baba wa watoto huo alisema kwamba, hakika Tanzania na Serikali ya Rais Kikwete inaongoza kwa unyanyasaji wa haki za wanawake na watoto, huku akiwa na mabangao  yalisomekwa kwamba, "Baba yangu yuko wapi???,Where is my Daddy!!!.
Hata hivyo taarifa zilizonaswa na Habarimpya.com zinadai kwamba kada huyo wa Chadema alikamatwa na kupewa mateso makali akiwa Kituo Kikuu cha Polisi  kwa muda wa siku mbili, ili ataje watu alioshirikiana nao katika tukio la kumwagia kijana mmoja tindi kali katika uchaguzi mdogo wa Igunga.
"Nikweli Huyu jamaa alikamatwa lakini mpaka hivi sasa hayupo hapa kituoni, ameondolewa asubuhi na mapema kuelekea Igunga ilipo kesi yake chini ya ulinzi mkali wa Jeshi la Polisi"chanzo cha ndani ya Jeshi la Polisi kilisema.
Habarimpya.com ilimtafuta Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania Advera Senso na alipopatikana  alisema kwamba Joyce Kiria anaipotosha umma wa watanzania.
"Kuhusu upooshaji wa Joyce Kiria inasikitisha kuona kwamba huyu mama anataka kuingilia mambo ya kisheria na kutaka kuipotosha jamii kwamba hajui mumewake juko wapi,pia analenga kuichochea jamii kwamba anayetuhumiwa kutenda uhalifu akikamatwa familia yake iandamane,tendo ambalo pia ni kosa la jinai,aidha anatakiwa kuheshimu haki za watoto na kuacha kuwatumia kama kinga ya kutetea watu wanaotuhumiwa kutenda uhalifu"alisema Senso.


No comments:

Post a Comment