Find us on facebook

Pages

Follow Me.

Tuesday, June 18, 2013

HAYA NDIO MAPENDEKEZO YA BAJETI YA KAMBI YA UPINZANI 2013/2014

MAPENDEKEZO YA BAJETI 2013/14 YA KAMBI YAUPINZANI
i. Sheria ya Kodi ya Mapato, SURA 332.
Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inapendekeza kiwango cha chini cha kutoza kodi ya mapato ya ajira kwa mfanyakazi (PAY AS YOU EARN) kishuke kutoka asilimia 14 hadi asilimia 9 ya mshahara wa mfanyakazi.

ii. 
Sheria ya Ushuru wa Bidhaa, SURA 147. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inapendekeza kufutwa kwa mapendekezo ya kuongeza kodi kwenye bidhaa za mafuta. Viwango vya sasa vya kodi na ushuru vibakie.

Kambi Rasmi ya Upinzani inapendekeza kodi mpya kwenye matumizi ya simu isikubaliwe na ibaki asilimia 12 kama ilivyokuwa zamani.

iii. 
Sheria ya Ushuru wa Mafuta, SURA 220.Katika sheria hii, Serikali inapendekeza kuongeza kiwango cha ushuru wa mafuta (fuel levy) kutoka shilingi 200 kwa litahadi shilingi 263 kwa kwa lita sawa na ongezeko la shilingi 63 kwa lita. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni haikubaliani na pendekezo hili kwani lina madhara makubwa kwa maisha ya wananchi kwa kuwa linaongeza gharama za maisha kama vilekupanda kwa nauli, bei za vyakula nk. Hivyo Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inapendekeza kufutwa kabisa kwa ushuru mpya wa mafuta.

iv. Sheriaya Petroli ( Petroleum Act) SURA 392.Katika sheria hii, Serikali inapendekeza kuanzisha tozo ya mafuta ya Petroli (petroleum levy) ya shilingi 50 kwa lita ambayo itakusanywa na Mamlaka ya Mapato (TRA) kwa ajili ya kugharamia mahitaji ya Wakala wa Umeme Vijijijni (REA). Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inayoongozwa na CHADEMA inapendekeza kufutwa kabisa kwa tozo ya mafutaya petroli ili kuwapunguzia wananchi ukali wa maisha. Fedha za kwenda REA zipatikane kutoka kwenye kupunguza misamaha ya kodi.

Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ina mapaendekezo mengine ya kikodi kama ifuatavyo:

1. Kuondoa ongezeko la Kodi kwenye ngano, ili kupunguza mfumuko wa bei kwenye bidhaa zitokanazo na ngano kama vile chapatti, mikate, maandazi nk.

2. Kupunguza misamaha ya kodi hadi asilimia moja ya pato la Taifa

3. Kupanua wigo wa kodi kwa kuanzisha tozo ya maendeleoya michezo (Sports Development Levy) ili kukuza michezo nchini na kugharimia timu za zinazowakilisha taifa katika michezo ya kimataifa. VAT inayolipwa hivi sasa kutoka viingilio vya michezo irekebishwe na kuwa ‘sports development levy’.

4. Kuongeza wigo wa kodi kwa kuanzisha tozo ya asilimia moja(1%) kwa bidhaa zote zinanazoingizwa nchini kutoka nje na tozo ya asilimia sifuri nukta tano (0.5%) kwa bidhaa zote zinazouzwa nje ya nchi kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya reli hapa nchini. (Railways Development levy on imports and exports).

5. Kambi ya Upinzani Bungeni inapendekeza kwamba kwa kuwa utaratibu wavitambulisho vya taifa umeanza na tayari sehemu fulani ya wananchi wamepewa vitambulisho na kwa kuwa kwa kupitia mfumo wa TIN na usajili wa magari kuna watanzania wengi sana wana rekodi za kikodi ni vema sasa sheria ya kodi ya mapato sura 332 ifanyiwe marekebisho ili kulazimisha kila mwananchi ajaze ‘tax return’ awe au asiwe na kipato.

6. Kambi ya Upinzani Bungeni inapendekeza kwamba mfumo wa VAT ‘zero rating’katika jedwali la Kwanza ufutwe na badala yake kwa bidhaa zenye umuhimu na zilizopo kwenye jedwali la kwanza zipelekwe jedwali la tatu kama ‘specialrelief’.

7. Kambi ya Upinzani inapendekeza sheria ya Uwekezaji nchini, TIC, ifanyiwe marekebisho ili Misamaha yote ya kodi iwekwe wazi na kukaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (Transparency and Audit of Tax exemptions)ili kudhibiti matumizi mabaya ya misamaha ya kodi.

8.Kambi ya Upinzani Bungeni inapendekeza mabadiliko ya Sheria yaMawasiliano (EPOCA) ya mwaka 2009 ili kuipa TCRA mamlaka ya kufanya ukaguzi wa uwekezaji unaofanywa na kampuni za simu hapa nchini kwa lengo la kuzuia ukwepaji kodi unatokana na kudanganya gharama za uwekezaji.

9. Kambi ya pinzani inapendekeza kuwa tozo mpya kwenye mobile money transfer litumike iwapo tu tozo kama hili litawekwa kwenye utumaji fedha kwa njia za benki na njia nyinginezo. Vinginevyo tozo hili ni la kibaguzi na linapendelea watu wenye uwezo mkubwa dhidi ya wanyonge na hivyo tunatoa wito kuwa pendekezo hili lisikubaliwe na Bunge.

10. Kambi ya Upinzani Bungeni inapendekeza Bunge litunge sheria kudhibiti matumizi ya ‘tax havens’ yanayofanywa na kampuni za uwekezaji na haswa kwenye sekta za Mawasiliano, Madini, Mafuta na Gesi na nyinginezo. Tanzania ijondoe katika mikataba yote yakikodi na nchi ambazo ni ‘tax havens’

No comments:

Post a Comment