Find us on facebook

Pages

Follow Me.

Sunday, June 23, 2013

KINACHODAIWA NI MBINU CHAFU DHIDI YA CHADEMA NDIO HIZI HAPA:

PRESS MAKAO MAKUU YA CHADEMA LEO TAREHE 23/06/2013
Habari za Jumapili WanaJF. Tuko live kuwaletea yatakayozungumzwa muda si mrefu hapa Makao Makuu ya CHADEMA Mtaa wa Ufipa, Kinondoni Jijini Dar es Salaam.
Ni Mkutano wa ghafla juu ya harakati chafu zinazoendelea kufanywa na Serikali, CCM, na Jeshi la Polisi dhidi ya Chama chetu. Karibuni sanaPress imeanza yuko Prof. Abdallah Safari na Mh. John Mnyika ndio wako meza kuu. Prof safari anaanza kuzungumza.
Anasema Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Dar es salaam Mh. Henry Kileo amekamatwa juzi na kunyimwa dhamana akidaiwa kuhusika na kesi ya Tindikali. 
Mpaka sasa wameshakamatwa vijana zaidi ya 5 kuhusiana na tuhuma hizo. Pia anasema kwa sasa wanapanga kuwakama M/kiti Mh. Mbowe, Dr.Slaa, Mnyika na Tundu Lissu.
Anasema Viongozi wote wa CHADEMA Mpaka sasa wameshashtakiwa kwa makosa ya jinai. Anasema kwenye sheria inaruhusiwa kujenga dhana. 
Anashangaa kwanini Viongozi wa Chama cha Upinzani CHADEMA, wamekamatwa wakati hata katika hukumu ya Igunga Hakimu alihukumu Rage akamatwe lakini mpaka sasa Rage hajawahi kukamatwa hata mara moja. Anasema Kileo amekamatwa Dar amepelekwa Mwanza na hatimaye Tabora.
Anasema watapeleka jopo la wanasheria kushughulikia kesi hii. Amamaliza anamkaribisha Mnyika sasa.
Mnyika anasema Mawakili wanaotangulia leo kwenda Tabora ni Wakili Prof. Abdallah Safari, Peter Kibatara na Henry Mwanaliela.
Anasema Mawakili watakaoongezeka baadae ni Mabere Marando, Nanyoro Kicheere, Tundu Lissu.
Mnyika anasema njama hizi ni za kisiasa na zimepangwa kwa vikao mbalimbali kwa mujibu wa taarifa zao walizonazo.
Anasema vinara wa mkakati huu ni Mwigulu Nchemba Naibu Katibu Mkuu CCM Bara na Advocate Nyombi Afisa Mwandamizi wa Jeshi la Polisi. Anasema lengo la kuwakamata vijana hawa ni kama chambo tu lakini wanaotafutwa ni viongozi wakuu wa Chama. 
Mnyika anasema alikamatwa kijana Evodius tarehe 2, Aprili huko kagera na wakamweka mahabusu siku 3 bila dhamana, akapelekwa Mwanza nako akaa mahabusu siku 4, wakamsafirisha kwa ndege kuja Dar es salaam. 
Muda waote akiwa mikononi mwa jeshi la Polisi alipigwa sana na akiwa Dar es salaam alipelekwa Makao Makuu na kufungiwa ndani akiwa na Advocate Nyombi na hapo aliteswa kwa shoti ya umeme sehemu za siri wakimlazimisha akiri kwa kuandika maelezo kuwa waliohusika na tukio la tindikali ni Mbowe,Slaa,Mnyika na Tundu Lissu.
Kijana mwingine anaitwa Rajabu alikamatwa Dodoma akateswa lakini baadae alipoonyesha kukataa aliahidiwa milioni 30 na akaahidiwa kuwa baada ya kesi asiwe na wasiwasi kwani atasaidiwa kama ambavyo wanamsaidia kijana Ludovick.
Mnyika anashangaa kwanini Nguvu kubwa inatumika namna hii kuhusu swala la Tesha ambaye anatumika kama bango na CCM lakini huko huko Igunga Wakala wa CHADEMA Mbwana Masoud aliuawa kikatili na hakuna anayeshughulikia swala hilo tena.
Anashangaa kada ya CCM aliyemchinja kwa msumeno wa nyororo Ndugu Mbwambo na hatimaye kada huyo kutoroka akiwa mikononi mwa Polisi lakini hajakamatwa tena na wala hakuna polisi aliyechukuliwa hatua kwa tukio hili. 

No comments:

Post a Comment