Find us on facebook

Pages

Follow Me.

Saturday, June 15, 2013

PICHA ZA MATUKIO MLIPUKO WA BOMU ARUSHA LEO HII:SAMHANI KWA PICHA HIZI.

 Watu wawili wanahofiwa kupoteza maisha na wengine
wengi kujeruhiwa kutokana na mlipuko wa bomu lililolipuka kwenye mkutano wa CHADEMA katika eneo la Soweto, kata ya Kaloleni jijini Arusha, wakati wa kufunga kampeni za uchaguzi wa madiwani katika maeneo ya jiji hilo.
 Waliojeruhiwa wamekimbizwa katika hospitali za Seliani na Mount Meru ambapo baadhi ya watu waliojitolea wanashirikiana na Madaktari na Wauguzi wa hospitali hizo kutoa huduma ya kwanza.
Kamanda wa polisi mkoani humo, Liberatus Sabas yupo katika moja ya hospitali hizo.

 Bomu hilo linaelezwa kuwa lilitupwa kwenye mkusanyiko wa watu, lilipuka mwendo wa saa kumi na mbili na robo jioni wakati mkutano huo ulipokuwa umekwisha na shughuli ya kukusanya michango ikiendelea.
Viongozi wa juu wa CHADEMA, Freeman Mbowe na Godbless Lema walikuwepo na wameendelea kuwepo kwenye eneo baada ya mlipuko huo.





No comments:

Post a Comment