Find us on facebook

Pages

Follow Me.

Monday, August 5, 2013

HUU NDIO UKWELI KUHUSU SHOMARI KAPOMBE

Habari zenu wapenzi wa Soka Tanzania,

Nimejiunga hapa ili niweze kutoa majibu kwa maswali yoyote kuhusu suala la mchezaji Shomari Kapombe aliye chini ya mwongozo wangu. Nimeamua nifanye hivi baada ya
kuona magazeti ya Tanzania yakipotosha mambo mbalimbali kuhusu kijana huyu, mimi mwenyewe na nini mipango yake. Pia naelewa waTanzania wanashauku ya kujua mchezaji anaendelea vipi.

Ni muhimu muelewe kwamba, kama siwezi kujibu swali ni kwasababu aidha inabidi niwe nimeshawataarifu Simba kwanza (kama wamiliki wa mchezaji) au ni kwamba tu siwezi kujibu hilo swali, na ikiwa hivyo nitatoa sababu.

Naomba pia muelewe kwamba mimi nimeishi huku miaka mingi (Uholanzi na Uingereza), nimecheza mpira na ninaelewa mahitaji yake, kwahiyo nimejipanga vizuri sana kumweka mchezaji yoyote yule katika mazingira mazuri ili afanikiwe. Ninafanya kazi na watu wanaojua kazi zao. Ninafanya yote haya nikiwa na ufahamu wa vikwazo nilivyopitia mimi kutokana na kutokuwa na mwongozo mzuri na kushindwa kufanikiwa kama mcheza mpira katika ngazi za juu. Ninatumia uzoefu wangu huo kuhakikisha Tanzania inapiga hatua.

Inabidi tukubali kwamba, waTanzania wengi tunapenda short-cut na kuharakisha mambo ili tufanikiwe maishani. Mimi nipo kuhakikisha tunafanya mambo kwa mwendo mzuri wenye kujenga na si kulipua. Kwa watu waliokuwa wanapakazia kijana ametumwa sembe, naomba mujiheshimu. Mimi ni Mhandisi katika kampuni kubwa tu na ninaridhika na ninachopata, sihitaji short-cut na ninawahakikishieni mchezaji yoyote ninayemchukua namweleza asikubali kutumika kwa vitu vya kijinga namna hiyo.

Nawakaribisheni mtiririke na dukuduku zenu. Ninachoweza kusema ni kwamba, kijana ameshacheza mechi mbili (mechi ya kwanza siku 10 baada ya kufika hapa, na mechi ya pili jumamosi iliyopita). Mechi ya kwanza alipewa offer 2 tayari na mechi ya pili nasubiri feedback kutoka scout wa Hispania aliyependezwa na mchezaji. Kuhusu offer zilizopo, swali ni je, ili tusonge mbele tunaangalia maendeleo ya mchezaji na taifa la Tanzania au maendeleo ya mchezaji na timu ya Simba au faida kwa Simba tu.

Karibuni,
Denis

P.S,
Nimeamua nije hapa kwasababu naona kuna watu wanatoa habari magazetini ambazo sio za kweli na zinanifanya mimi nionekane ni mbabaishaji. Nimeongea mara moja tu na mwandishi Saleh Ally wa Championi baada ya yeye kunipigia simu (infact alinibeep, mi nikapiga simu nikakutana na maswali)...yaani nimechajiwa mimi kwa interview ambayo sikuomba. 

Pili Mtangazaji mmoja wa redio ile ya Lady Jay Dee alinipigia simu. Yule jamaa nilimwambia asinirekodi lakini akafanya hivyo akarusha habari. Alirusha habari kiuchochezi maana niliongea nae dakika 11 lakini akachagua acheze kipande kitakachomfaa yeye. Kama angeamua kucheza interview yote, mngeona jinsi alivyo mnafiki. Huyu ni mtu aliyeniahidi kunipatia video za wachezaji mbalimbali ninaowafuatilia Tanzania. Hakufanya hivyo. Alinipigia simu siku hiyo akiwa hajui kwamba mimi ndio nilimwomba hizo video miezi michache kabla.

Naomba pia niwaambie kwamba sijawahi kusema kijana anaenda kucheza FC Twente wala sikutaja timu yoyote ile wakati nawaomba Simba ruhusa wala Taifa Stars. Lakini kijana kaonekana na mascout wamemuona, na nimehakikisha anaonekana sababu najua ninachofanya. Sina haja ya kuongea na gazeti lolote sababu sitaki hiyo publicity na kwasabu mimi ni mtendaji na si muongeaji.

No comments:

Post a Comment