Find us on facebook

Pages

Follow Me.

Sunday, October 13, 2013

MWANDISHI WA HABARI UFOO SARO WA ITV NA RADIO ONE APIGWA RISASI PAMOJA NA MAMA YAKE.

Taarifa za mwanzo za kusikitisha ambazo tumezipata hivi punde zinasema mtu mmoja anayedhaniwa kuwa mume au mchumba wa mwandishi wa habari wa ITV na Radio One Ufoo Saro amefanya mauaji ya kutisha na
yeye mwenyewe kujiua.
Akizungumza na radio one kamanda wa polisi wa mkoa wa kipolisi wa Kinondoni kamanda Wambura amesema tukio hilo limetokea majira ya alfajiri ya leo.
Kamanda wambura ameongeza kuwa mwanaume huyo anafanya kazi Umoja wa Mataifa (UN) huko Sudani ila bado haijafahamika kwamba anafanyia kitengo gani (japo kwa habari za mtaani zinasema mtu huyo ni mwanajeshi ila bado hazijathibitishwa
                       Kamanda Wambura anasema inasemekana kulikua kuna ugomvi kati ya wawili hao ambapo walishindwa kuelewana na ndipo walipoamua kwenda kwa mama mzazi wa Ufoo Saro (mama mkwe) na ndipo mwanaume huyo alipomshutumu mama mkwe wake kwamba anamtetea mwanae ndipo alipotoa bastola na kumpiga mama yake na Ufoo Saro Risasi ya kichwa na kumuua papo hapo na kisha akampiga Ufoo Saro risasi ya mbili moja ya tumboni na ingine ya mguuni na kudhani kwamba amemuua kumbe amemjeruhi tu kisha kujipiga mwenyewe risasi ya kidevuni na kufariki dunia hapo hapo.

                           Source: Breaking News - Radio One

No comments:

Post a Comment