Saturday, May 18, 2013
ANACONDA TEAM YAZIDI KUWA KUBWA.MASTAA WAONGEZEKA.
Ukiangalia katika picha hao ndio baadhi ya wasanii wanaomuunga mkono JIDE katika harakati za upingaji juu ya wanamziki kunyonywa katika kazi zao.
huyu mheshimiwa alijitoa kwa sababu amabazo alizitaja mwenyewe,sasa mashabiki wake inaonekana kumpinga vikali kwa huo uamuzi aliouchukua ikiwemo kupewa matusi na mashabiki wake.
MANENO YA ESMA DADA YAKE DIAMOND KUHUSU NDOA YAKE.
Esma Abdul ambae ni dada yake mwimbaji staa wa Tanzania, Diamond Platnums, amesema wamejiandaa vizuri kwa ajili ya harusi ya Diamond ambae anatarajiwa kumuoa mtangazaji wa TV aitwae Penny.
Esma ambae anaishi nyumba moja na kaka yake amesema, "Tumemkubali sana wifi yetu na tunampenda kwa sababu mtu yeyote mimi nitakaetambulishwa siwezi nikamkataa, manake nikimuingilia kwenye mapenzi yake na yeye ataniingilia kwenye mapenzi yangu."
Huu ni mwezi wa tano toka Esma amjue wifi yake ambae ni Penny, anasema nyumbani amekubalika na mipango ya harusi inaandaliwa japo hajui ni lini itafanyika, manake hiyo ni siri kwa sasa.
Zaidi ya wiki tano zilizopita, Diamond aliongea na kusema ndoa yake imekaribia kufungwa na huyo mkewe mtarajiwa ambae ni mjamzito lakini pia akathibitisha kumnunulia gari la kutembelea aliloliagiza nchini Japan - Hyundai IX 35.
Mpaka sasa Mwimbaji Diamond Platnums ambae aliongoza kwa kuwa msanii wa Tanzania alieandikwa sana kwenye internet 2012, ameshaingia kwenye headlines za kuwa mapenzini na mastaa wa kike Tanzania kipindi cha nyuma kama Jokate, Wema Sepetu na wengine.
Subscribe to:
Posts (Atom)