Gervas Mwatebela, Dar es Salaam
Wasomaji wetu leo tumeamua kuangazia suala dogo tu katika utalii wa ndani kwa kutazama baadhi ya magari aliyotumia Baba wa Taifa na Rais wa kwanza wa Tanzania Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wakati wa harakati za Uhuru na baada ya Uhuru mpaka alipofariki Oktoba 14,1999. Maelezo ya makala haya ni kwa mujibu wa nyaraka zilizopo Makumbusho ya Taifa, Dar es Salaam hasa kuhusiana na magari na miaka ya magari yalipotumika. Fuatana nasi.
1.AUSTIN MORRIS A-40
Gari aina ya Austin Morris A-40 lilitengenezwa nchini Uingereza kati ya mwaka 1940 – 1950. Ni gari la kwanza kutumiwa na