Wagonjwa wawili wameondolewa bughdha ya kutumia madawa ya kupunguza makali ya ukimwi maishani mwao baada ya kufanyiwa upasuaji na kupandikiziwa uboho wan binadamu au (Bone marrow), hatua inayosemekana kuondoa virusi vya HIV mwilini mwao.
Mgonjwa mmoja amesemekana kukaa kwa miezi minne bila ya kutumia madawa ya kupunguza makali ya ukimwi bila ya dalili ya kurejea kwa uogonjwa huo.
Matokeo ya utafiti huo yaliwasilishwa katika mkutano wa kimataifa kuhusu maswala ya Ukimwi.Madaktai waliofanya utafiti huo katika hospitali ya matibabu kwa wanawake ya Brigham nchini Marekani, wanasema ni