Mwanadada Judith Mbibo aka Lady Jaydee usiku wa kuamkia Jumamosi ya June 15 amefanikiwa kuweka historia kwenye muziki wa Tanzania kwa kulijaza eneo zima la Nyumbani Lounge alipokuwa akifanya show yake ya kuadhimisha miaka 13 tangu aanze muziki.
Hii imedhihirisha kuwa majina anayojiita mwanadada huyu ni ya halali kabisa na yanamfaa kwani tafauti na watu walivyodhan palijaa watu hadi wakaanza kubebana ama kwa hakika huyu ni komando,anaconda hebu anagalia picha mdau utakubaliana na mimi
Hivi ndivyo hali ilivyo ndani ya Ukumbi huu wa Nyumbani Lounge,Namanga jijini Dar es Salaam ambapo ambapo jana lilikuwepo bonge moja la show la Mwanadada mkongwe kwenye tasnia ya muziki hapa nchini,Lady Jay Dee ambaye anatimiza miaka 13 tangu alipoanza kazi yake ya muziki.katika show hii wanamuziki mbali mbali wamepanda jukwaani akiwepo Mh. Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini,Mh. Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu.