Umoja wa Mataifa umesema takriban watoto elfu tisini na tatu wameuawa nchini Syria tangu kuanza kwa mapigano nchini humo.
Kwa mujibu wa takwimu hizo, idadi hiyo imeongezeka kwa zaidi ya
elfu thelathini, tangu umoja huo ulipotoa takwimu zake Januari mwaka huu.
Ripoti hiyo imesema kuwa watu elfu tano hufa nchini Syria kila mwezi tangu Julai mwaka uliopita
Hata hivyo takwimu hizo huenda sio idadi kamili na Umoja wa Mataifa umesema huenda idadi ya waliouawa huenda ikawa kubwa zaidi, kwa kuwa vifo vingi havijaripotiwa.
Asilimia themanini ya waliouawa ni wanaume, lakini Umoja huo umeongeza kusema kuwa tayari umethibitisha kutokea kwa vifo vya zaidi ya watoto elfu moja mia saba ambao wako chini ya umri wa miaka kumi.
Vile vile, kuna ripoti kuwa watoto wengine waliteswa kabla ya kuuawa kinyama.
Afisa mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya haki za binadam Navi Pilllay, amesema wamepokea ripoti ya kutokea kwa mauaji ya familia nyingi wakiwa na watoto wao, ishara kuwa vita vinavyoendelea nchini Syria vimegeuka kuwa janga kuu huku maelfu ya watu wakiendelea kuuawa kila siku.
Wakati huo huo, wanaharakati wa upinzani nchini Syria na shirika la habari la serikali wamesema kuwa makombora yaliyorushwa na wanajeshi wa waasi yameanguka katika uwanja mkuu wa ndege mjini Damascus.
Moja ya makombora hayo yaliyotengenezwa nyumbani, lilianguka karibu na barabara ya kurukia ndege na hivyo kulazimisha safari kadhaa za ndege kucheleweshwa kwa sababu za kiusalama.
Shambulio hilo ndilo la kwanza katika uwanja huo wa ndege ambao kwa sasa umezingirwa na wanajeshi wa serikali.
No comments:
Post a Comment