Find us on facebook

Pages

Follow Me.

Friday, May 17, 2013

WANAFUNZI WANAOJIUZA CBE NA UDSM MAJINA YAO HEWANI.

Wanafunzi wa kike wa chuo kikuu cha Dar es salaam [UDSM],Chuo cha elimu ya biashara [CBE]na chuo cha mamlaka ya Elimu na ufundi stadi [VETA],Dar es salaam ,wamefikishwa katika mahakama ya jiji samora wakidaiwa kufanya biashara ya kuuza mili yao. Washitakiwa hao waliokamatwa katika eneo la kona Baa Ambiance Sinza wilayani kinondoni ambao ni miongoni mwa wanawake 35 wanaodaiwa kufanya biashara hiyo na wote walifikishwa mahakamani hapo. Kesi hiyo ilikuwa chini ya hakimu Willian Mtaki ambapo muendesha mashitaka,bwana John Kijumbe,alisema wasichana hao walikamatwa katika mazingira tofautitofauti. Wanafunzi hao ni Yasinta Kilimo mwenye miaka 21 CBE mkazi wa upanga,Morin Masatu miaka 19 UDSM,mkazi wa kinondoni na mwanafunzi wa VETA aliyefahamika kwa jina moja la Khadija. “Nilikwenda pale baa kuchukua simu yangu ambayo ilipotea hivyo waliniita nikaichukue ndipo askari wa jiji wakanikamata,”Alisema Khadija akijitetea. Kwa mujibu wa bw. Kijumbe washitakiwa hao wamekosa dhamana baada ya kushindwa kutimiza masharti ya kila mmoja kuwa na wadhamini wawili au kulipa faini ya kulipa sh. 200,000. Kesi hiyo inatarajiwa kusikilizwa tena mei 28 mwaka huu,ambapo washitakiwa wote walipelekwa Segerea. Wakati huohuo, jeshi la Polisi mkoa wa kinondoni , limewakamata watuhumiwa 716 waliokuwa wakijihusisha na biashara ya kuuza miili kati yao wanaume 38 na wanawake 678. Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi mkoa wa kipolisi Kinondoni Charles Kenyela, alisema watu hao walikamatwa kwenye msako uliodumu kwa miezi sita kwenye maeneo mbalimbali ya Kinondoni. Maeneo hayo ni baa, kumbi za starehe, madanguro, sehemu za wazi katika ufukwe wa Bahari ya Hindi, na makaburini ambapo kati ya wanaume waliokamatwa wengine ni mashoga pamoja na wateja wa machagudoa. “Msako huo ulifanyika Maisha Club, Coco Beach, Barabara ya Tunisia , Travertine Hotel, Tandale Uwanja wa Fisi, Ambiance Club, Shekilango pamoja na Mwinanyamala” Alisema Kamanda Kenyela aliongeza kuwa , jeshi hilo pia limewakamata raia 12 kutoka nchini Ethiopia walioingia nchini bila kibali kati ya Mei 2 na 6, mwaka huu katika eneo la Kimara Mwisho na Tegeta Kibaoni. Alisema kukamatwa kwao kulitokana na taarifa walizozipata kutoka kwa raia wema waliowaona maeneo

T.I.D APOKEA MABANGO BAADA YA KUSUSA SHOO YA ANACONDA(LADY JAYDEE)


Wadau kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii wamemjia juu msanii mkongwe T.I.D ali maarufu kama mnyama.hiyo ni baada ya kususia shoo ya mwanadad JIDE inyotegemea kufanyika tarehe 31may.T.I.D anashutumiwa kufanya hicho kitu baada ya kushawishiwa na watu maarufu na wamiliki wa kituo kikubwa cha redio nchini.

Arafat.

arafat ngumi jiwe katika kashifa ya kuliwa kiboga baada ya kufamaniwa akimfanyia mtoto mambo hayo.

Mubaah Katela.

welcome to my blog.

LAMPARD SHUJAA WA MAGORI CHELSEA.

Mabao mawili ya Frank Lampard yaliifanya Chelsea kuibuka na ushindi wa 2-1 ugenini dhidi ya Aston Villa. Magoli hayo mawili aliyoyafunga Lampard ambaye ni nahodha msaidizi wa timu hiyo na timu ya taifa ya Uingereza, yamefanya avunje rekodi ya Bobby Tambling mchezaji wa zamani wa Chelsea na kuweka rekodi mpya ya kuwa mfungaji bora wa muda wote wa klabu hiyo ya mashariki mwa London baada ya kufikisha idadi ya kufunga jumla ya mabao 203 tangu aanze kuichezea The Blues. Chelsea walikuwa wageni kwenye uwanja wa Villa Park katika mechi ambayo ilikuwa na ushindani huku kadi mbili nyekundu zikitoka. Christian Benteke wa Aston Villa na Ramires wa Chelsea walipewa kadi nyekundu kwa nyakati tofauti. Kwa matokeo haya Chelsea sasa wanasalia kwenye nafasi ya tatu na pointi 72 huku Aston Villa wakiwa bado kwenye nafasi ya 13 na pointi 40. Michezo mingine ya ligi kuu ya England inayofikia tamati wiki ijayo itachezwa kwa nyakati tofauti hapo jumapili. Stoke City watakuwa wakipambana na Tottenham Hotspurs wakati Everton watakuwa nyumbani kuwakaribisha West Ham United. Kwingineko Fulham watawakaribisha Liverpool kwenye uwanja wa Craven Cottage huku Norwich wakitarajia kupapatauana na West Brom. Sunderland wao watakuwa wakicheza mchezo ambao kocha wao Paulo Di Canio ameuita mchezo wa fainali kwao dhidi ya Southampton,mchezo ambao utaamua hatima yao ya kushuka ama kusalia kwenye ligi kuu msimu ujao. Mabingwa Manchester United wao watacheza mchezo wao wa mwisho kwenye uwanja wa Old Trafford dhidi ya Swansea, mchezo ambao United watautumia kumuaga kocha wao Sir Alex Ferguson aliyetangaza kustaafu msimu ujao na pia watakuwa wakikabidhiwa rasmi kombe la ubingwa wa ligi kuu msimuu huu. Na mchezo wa mwisho QPR watakuwa wakipambana na Newcastle, mchezo ambao BBC Ulimwengu wa soka itakuwa ikutangazia moja kwa moja kuanzia majira ya saa kumi na moja na nusu jioni kwa saa za Afrika mashariki sawa na saa kumi na nusu Afrika ya kati.

VITA YASHIKA KASI NIGERIA.

Operesheni hiyo inakuja baada ya serikali kutangaza hali ya hatari katika majimbo ya Borno, Yobe na Adamawa Kaskazini Mashariki mwa nchi ambako watu 2,000 yatari wameuawa tangu mwaka 2009. Amri ya kutotoka nje kuanzia saa za jioni hadi asubuhi imetangazwa katika jimbo la Adamawa ili kukabiliana na wanamgambo hao. Mwandishi wa BBC katika jimbo la Adamawa anasema kuwa uamuzi huo unashangaza kwani hali ya usalama katika jimbo hilo sio mbaya ikilinganishwa na majimbo ya Borno na Yobe. Mnamo siku ya Alhamisi wanajeshi walivamia kambi za wanamgambo katika mbuga ya wanyama na ambayo inasifika kuwa moja ya ngome kuu za kundi la Boko Haram Msemaji wa jeshi la Nigeria Brigedia Generali Chris Olukolade, alisema kuwa watatumia uwezo wao wote wa kijeshi kukabiliana vilivyo na wapiganaji wa Boko Haram.

CD ZA UAMSHO MARUFUKU KUUZWA ZIPO NA ILUNGA.

Katika hali isiyo ya kawaida mjini Zanzibar cd za uamsho na zile za shekhe ILUNGA na mashehe wengine zimepigwa marufuku.Ni kwa kile kinachodaiwa kwamba CD hizo zinaleta uchochezi wa kidini ambao ni hatari kwa amani ya taifa na inasemakana ndo chanzo cha kulleta baina ya sintoelewana kati ya dini mbili waislamu na wakristo Nchini.

KUTOKA MTWARA.

Katika mji wa mtwara kulitegemewa leo kuwepo na maandamano ambapo mji huo umekumbwa na hofu kiasi kwamba baadhi ya biashara katika mji huo hazijafanyika.Mji huo umekuwa tulivu na polisi walionekana wakiranda randa katika mji huo.

MAGAZETI YA LEO IJUMAA TAREHE 17

MAGAZETI YA LEO IJUMAA TAREHE 17

KUTOKA MTWARA.

Katika mji wa mtwara kulitegemewa leo kuwepo na maandamano ambapo mji huo umekumbwa na hofu kiasi kwamba baadhi ya biashara katika mji huo hazijafanyika.Mji huo umekuwa tulivu na polisi walionekana wakiranda randa katika mji huo.