Friday, May 17, 2013
LAMPARD SHUJAA WA MAGORI CHELSEA.
Mabao mawili ya Frank Lampard yaliifanya Chelsea kuibuka na ushindi wa 2-1 ugenini dhidi ya Aston Villa.
Magoli hayo mawili aliyoyafunga Lampard ambaye ni nahodha msaidizi wa timu hiyo na timu ya taifa ya Uingereza, yamefanya avunje rekodi ya Bobby Tambling mchezaji wa zamani wa Chelsea na kuweka rekodi mpya ya kuwa mfungaji bora wa muda wote wa klabu hiyo ya mashariki mwa London baada ya kufikisha idadi ya kufunga jumla ya mabao 203 tangu aanze kuichezea The Blues.
Chelsea walikuwa wageni kwenye uwanja wa Villa Park katika mechi ambayo ilikuwa na ushindani huku kadi mbili nyekundu zikitoka.
Christian Benteke wa Aston Villa na Ramires wa Chelsea walipewa kadi nyekundu kwa nyakati tofauti.
Kwa matokeo haya Chelsea sasa wanasalia kwenye nafasi ya tatu na pointi 72 huku Aston Villa wakiwa bado kwenye nafasi ya 13 na pointi 40.
Michezo mingine ya ligi kuu ya England inayofikia tamati wiki ijayo itachezwa kwa nyakati tofauti hapo jumapili.
Stoke City watakuwa wakipambana na Tottenham Hotspurs wakati Everton watakuwa nyumbani kuwakaribisha West Ham United.
Kwingineko Fulham watawakaribisha Liverpool kwenye uwanja wa Craven Cottage huku Norwich wakitarajia kupapatauana na West Brom.
Sunderland wao watakuwa wakicheza mchezo ambao kocha wao Paulo Di Canio ameuita mchezo wa fainali kwao dhidi ya Southampton,mchezo ambao utaamua hatima yao ya kushuka ama kusalia kwenye ligi kuu msimu ujao.
Mabingwa Manchester United wao watacheza mchezo wao wa mwisho kwenye uwanja wa Old Trafford dhidi ya Swansea, mchezo ambao United watautumia kumuaga kocha wao Sir Alex Ferguson aliyetangaza kustaafu msimu ujao na pia watakuwa wakikabidhiwa rasmi kombe la ubingwa wa ligi kuu msimuu huu.
Na mchezo wa mwisho QPR watakuwa wakipambana na Newcastle, mchezo ambao BBC Ulimwengu wa soka itakuwa ikutangazia moja kwa moja kuanzia majira ya saa kumi na moja na nusu jioni kwa saa za Afrika mashariki sawa na saa kumi na nusu Afrika ya kati.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment