President Barack Obama wa Marekani tayari amemaliza ziara yake ya siku mbili Tanzania ambapo sehemu ya mwisho kuitembelea ilikua Ubungo Dar es salaam ambako aliidhinisha mpango wa serikali yake wa dola
bilioni saba kwa ajili ya kusaidia mradi wa umeme kwenye bara la Afrika.
Anakwambia huo mradi ni muendelezo wa sera za serikali yake katika kuhakikisha Afrika inakua na umeme wa uhakika mara mbili ya ilivyo sasa hivi ambapo ukikamilika, utawezesha ukuaji wa uchumi kwa kasi inayotakiwa.
Pamoja na Marekani kuidhinisha hiyo pesa kwenye mradi wa umeme, kundi la Wafanyabiashara Afrika litachangia dola za Kimarekani bilioni 9 kwa ajili ya huo mradi wa umeme ambao kwanza utajikita kwenye nchi za Tanzania, Kenya, Ethiopia, Ghana, Liberia na Nigeria.
Baada tu ya ziara ya Ubungo, President Barack Obama alisindikizwa Airport JK Nyerere na kuondoka kurudi Marekani kwa kutumia ndege binafsi ya Rais aliyokuja nayo Afrika na kuzitembelea nchi za Afrika.
No comments:
Post a Comment