Find us on facebook

Pages

Follow Me.

Sunday, May 26, 2013

LEO HII JIDE KUTINGA MAHAKAMANI.

Kutokana na kesi aliyofunguliwa mahakamani msanii Lady Jaydee
leo ndio siku Lady JayDee anatarajia kupanda kizimbani kwa mara ya kwanza baada ya kukabidhiwa hati ya mashtaka na kutakiwa kurudi mahakamani leo hii mei 27 .

Waandishi wa habari walishuhudia barua kutoka mahakamani hapo pamoja na nyakara zilizochapishwa na vyombo mbalimbali vya habari zikiwamo blogu zilizoelezea ugomvi wake kati ya Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga na Mkurugenzi wa Utafiti na Matukio Ruge Mutahaba.
“Hili ndilo shtaka lenyewe kwa hivyo sisi hatuwezi kusema chochote kwa sasa tunaelekea kwa mwanasheria wetu ili kuanza kuishughulikia kesi hii,” alisema Gadna Habash mume wa mwanamuziki huyo. 
Kabla ya kufika mahakamani hapo mchana, mwanamuziki huyo alitoa mada katika jukwaa la sanaa Basata ambako alizungumzia changamoto nyingi zilizopo katika kufikia mafanikio kwenye sekta ya muziki.
 
Wakati kesi hiyo inatarajiwa kuanza kusikilizwa Mei 27, siku nne baadaye Jaydee anasherehekea miaka yake 13 tangu aingie rasmi katika sekta ya muziki.

No comments:

Post a Comment