Find us on facebook

Pages

Follow Me.

Tuesday, June 4, 2013

GADDAFI ALIFICHA MALI AFRIKA KUSINI:

Wizara ya fedha ya Afrika Kusini inachunguza tuhuma kwamba mali ya thamani ya kama dola
bilioni moja ya Libya ilifichwa nchini humo.
Wakuu wa Libya wamedai kuna dhahabu, almasi na fedha taslim ambazo kiongozi wa zamani wa Libya, Kanali Gaddafi na familia yake, waliziweka Afrika Kusini.
Serikali ya Libya imekuwa ikijaribu kuzipata mali za Kanali Gaddafi katika sehemu mbali-mbali za dunia tangu alipofariki mwaka 2011.

Mwandishi wa BBC mjini Johannesburg anasema watu wengine wamekisia kuwa mali ya hayati Gaddafi ilioko nchi za nje inaweza kufika dola bilioni 80.

No comments:

Post a Comment