Find us on facebook

Pages

Follow Me.

Tuesday, June 4, 2013

SHERIA TETE YA VYOMBO VYA HABARI BURUNDI.

Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza, ameidhinisha kama sheria mswaada
unalenga kudhibiti utenda kazi wa vyombo vyua habari.
Wakosoaji wanasema kuwa Rais anashambulia uhuru wa vyombo vya habari.
Pia inawalazimisha waandishi wa habari kufichua chanzo cha habari yao pamoja na kuwatoza faini ya zaidi ya dola elfu tano.Sheria hiyo inaharamisha waandishi wa habari kuripoti kuhusu maswala yanayoweza kuhujumu usalama wa kitaifa, utulivu wa umma na uchumi.
Vyombo vya habari pamoja na mashirika ya umma , yamelalamika kuhusu sheria hiyo wakisema kuna utata kuhusu ilivyotungwa na kuwa ni tisho kwa uhuru wa vyombo vya habari.
Sheria hii insemekana kuwa tata na inakuja wakati vyombo vya habari nchini Burundi vinakabiliwa na wakati mgumu.
Hassan Ruvakuki ni mmoja wa waandishi wa habari ambaye amekuwa akizuiliwa kwa muda mrefu huku baadhi ya waandishi wa habari wakilalamika kuhusu kunyanyaswa na polisi. Ruvakuki alikamatwa kwa madai ya ugaidi na kupewa kifungo cha maisha lakini kilipunguzwa hadi miaka mitatu gerezani baada ya kukata rufaa. Ni mwandishi haba ri wa shirika la habari la RFI

No comments:

Post a Comment