Find us on facebook

Pages

Follow Me.

Sunday, June 2, 2013

HIZI NDIZO SABABU 12 ZA CCM KUKATA RUFAA DHIDI YA LISSU.

Chama cha Mapinduzi kimeeleza hoja 12 katika kesi ya rufaa ya kupinga ushindi wa ubunge wa Mbunge
wa Singida Mashariki Tundu Lissu.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, Mwanasheria wa chama hicho, Glorious Luoga ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho (Nec), alisema katika kesi hiyo yenye shauri namba 1 ya 2010, waliwasilisha sababu za kukata rufaa Mei 7, mwaka huu.

Alisema mambo hayo ni ya kiutendaji ya kawaida na yalifanywa na yeye bila Katibu Mkuu kushirikishwa kwani hayakuhitaji ushiriki wake.

“Hapo katikati mahakama ilichelewa kutoa nakala ya hukumu na mwenendo wa mashitaka ambao tuliupokea Machi 8 mwaka huu ndani ya siku 90 toka hapo tukawasilisha Memorandum of Appeal Mei 7 mwaka huu” alisema.

Mwanasheria huyo alisema wamekata  rufaa Mahakama ya Rufaa  kutokana na hukumu iliyotolewa kuwa na makosa mengi ya kisheria.

Alizitaja hoja hizo ni kuwa pamoja na Jaji kufuta baadhi ya vifungu vya maombi ya kutengua uchaguzi na kuruhusu maombi kuendelea kusikilizwa wakati vifungu hivyo vimefutwa, Jaji alikuwa akiwazuia mashahidi kueleza baadhi ya ushahidi wao na pia alikuwa akifuta katika kumbukumbu baadhi ya maelezo ya mashahidi na  alikataa kuitwa kwa msimamizi wa uchaguzi kama shahidi muhimu wa kuhojiwa.

Nyingine ni Jaji alikataa kutumia ushahidi wote uliotolewa na mashahidi ambao ni wanachama wa CCM akidai ni wapambe, alikataa kukubali ushahidi uliotolewa na wanachama wa Chadema dhidi ya Lissu na akawaita ni “Turn court”, pia alikataa kupokea ushahidi wa CD akidai kuwa ushahidi huo Tanzania unakubalika katika kesi za jinai tu.

Alisema Jaji pia alikubali viapo vya mawakala ambavyo viliapwa kinyume cha sheria.

Alimtaka Lissu kujipanga na kesi iliyopo mbele yake badala ya kuingiza siasa.

Akizungumzia kuhusu tuhuma za CCM kulipa gharama za kesi hiyo, alisema
kesi zote zilizofunguliwa kupinga matokeo ya uchaguzi zimegharamiwa na CCM kwani ni wajibu wake hata kama zimefunguliwa na wanachama.

Alitolea mfano kuwa hata Chadema iligharamia kesi ya Deus Mallya ambaye alikuwa dereva wa aliyekuwa Mbunge wa Tarime Hayati Chacha Wangwe.
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment