Find us on facebook

Pages

Follow Me.

Sunday, June 2, 2013

UKUTA WA MNARA WA MAJI WAANGUKA PEMBA WATU WAPOTEZA MAISHA.

JUMLA ya watu watatu wamefariki dunia papo hapo na watatu kujeruhiwa  baada ya kuangukiwa na ukuta wa mnara wa tanki la maji uliopo
Machomanne Chake Chake Pemba, leo saa tatu  asubuhi.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Pemba, Suleiman Hassan Suleiman, amesema kuwa, merehemu hao walifikwa na mauti wakiwa katika kazi ya kuteremsha ukuta wa mnara wa tanki la maji ambao walikuwa wameshaukata.
Kamanda alisema kuwa idadi ya mafundi waliokuwepo kazini hapo walikuwa ni 12 ambapo watatu wamepoteza maisha papo hapo na watatu kujeruhiwa na kulazwa katika hospitali ya Chake Chake na wengine sita walikimbia na jeshi la polisi liko katika utaratibu wa kuwatafuta kwa ajili ya kuelewa hali zao.
Kamanda Suleiman aliwataja marehemu hao kuwa ni Juma Rashid Juma (35) mkazi wa Chanjaani, Suleiman Mohammed Abdiadi 'maarufu kama Golo' (55) mkazi wa Kwale na Salum Muhidini Vuai 'Bandudu' (35) mkazi wa Madungu wote wakazi wa wilaya ya Chake Chake mkoa wa Kusini Pemba.
Na majeruhi katika ajali hiyo ni pamoja na Jackson John (26) mzaliwa wa Iringa na mkazi wa Msingini, Ali Saleh Ali (35) mkazi wa Michakaeni na Yohana Richard (25) mkazi wa Machomanne Chake Chake Pemba.


No comments:

Post a Comment