MKE wa Kada wa Chama Cha
Maendeleo na Demokrasia (Chadema) Joyce Kiria leo amejikuta katika wakati
mgumu, baada ya kujitokeza mbele ya vyombo vya habari akiwa na watoto wake
wawili wadogo,huku akimwaga machozi kutokana na kile alicho elezwa kwamba
anamtafuta mumewake.
Mwanadada huyo ambaye ni
mwanaharakati na mtetezi wa haki za wanawake amekuwa mhanga wa kazi yake ya
utetezi wa wanawake baada ya Jeshi la Polisi nchini Tanzania kumficha mumwewe
Henry Kileo.
Akizungumza na Habarimpya.com
jijini Dar es Salaam, Kiria ambaye ni Mtangazaji wa kipindi cha Wanawake
LIVE,kinachorushwa katika kituo cha Televisheni ya Chanel 5 (EATV) pamoja na
DSTV, alisema kwamba mumewe ambaye ni kada wa Chadema aliitwa Polisi tangu siku
ya Ijumaa iliyopita na kuwekwa rumande, lakini walipofuatilia tukio hilo
wakaambiwa kwamba hajulikane alipo.
"Mume wangu aliitwa na
jeshi la polisi tangu siku ya Ijumaa ya wiki iliyopita na alipofika kituo hapo
aliamuriwa azime simu yake na kuwekwa kizuizini,tangu siku hiyo sijamuona mume
wangu na sijui alipo, nikipiga simu yake haipatikani tulipokwenda Kituo Kikuu
cha Polisi Dar es Salaam nikaambiwa kwamba hayupo kituoni hapo na hajulikani
alipo"alisema Kiria na kuongeza huku akibubujika machozi:.
Leo tena nimekwenda kituoni
hapo nikapewa jibu lisiloeleweka, kwamba Mumwe wangu alikuwepo hapo asubuhi
lakini ameondolewa na kwamba haijulikani alipopelekwa, huku mtoa taarifa akidai
kwamba pengine amepelekwa Tabora, sasa mimi nishike lipi ndugu zandu sijui mume
wangu alipo na ameniacha na watoto wadogo kama mnavyo waona hapa".
Kiria alimtaka Rais Jakaya
Kikwete pamoja na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Said Mwema kumweleza mumewe
alipo, kwa sababu wasaidizi wao wameshindwa kuweka wazi alipo baba watoto wake.
"Haina haja ya wao
kunificha alipo mume wangu, hata kama wamesha muua waniambie ilipo maiti yake,
ili nikamchukue na kumzika na kama yuko hai waniambie alipo ili nimpelekee hata
maji ya kunywa,sipingani na sheria pengine amefanya kosa kweli, lakini kila
mtuhumiwa ana haki ya kuwasiliana na familia yake, kwanini wanampa mumewangu
mateso makali kama hayo".Kaniacha na watoto wadogo
Linkon (miezi 4) na Liston (miaka 2) mimi hawa watoto nitawapa nini katika
maisha yangu, kama baba yao bado yuko hai waniruhusu nimuone, ili angalau
anishauri jinsi ya kuwalea watoto wake"aliongeza Kiria.
Kiria ambaye aliandamana na
ndugu zake wengine wanaoishi nyumbani kwake wakiwa na mabango yaliyokuwa ujumbe
wa kutafuta baba wa watoto huo alisema kwamba, hakika Tanzania na Serikali ya
Rais Kikwete inaongoza kwa unyanyasaji wa haki za wanawake na watoto, huku
akiwa na mabangao yalisomekwa kwamba, "Baba yangu yuko wapi???,Where
is my Daddy!!!.
Hata hivyo taarifa
zilizonaswa na Habarimpya.com zinadai kwamba kada huyo wa
Chadema alikamatwa na kupewa mateso makali akiwa Kituo Kikuu cha Polisi
kwa muda wa siku mbili, ili ataje watu alioshirikiana nao katika tukio la
kumwagia kijana mmoja tindi kali katika uchaguzi mdogo wa Igunga.
"Nikweli Huyu jamaa
alikamatwa lakini mpaka hivi sasa hayupo hapa kituoni, ameondolewa asubuhi na
mapema kuelekea Igunga ilipo kesi yake chini ya ulinzi mkali wa Jeshi la
Polisi"chanzo cha ndani ya Jeshi la Polisi kilisema.
Habarimpya.com ilimtafuta Msemaji wa Jeshi la
Polisi nchini Tanzania Advera Senso na alipopatikana alisema kwamba Joyce
Kiria anaipotosha umma wa watanzania.
"Kuhusu upooshaji wa
Joyce Kiria inasikitisha kuona kwamba huyu mama anataka kuingilia mambo ya
kisheria na kutaka kuipotosha jamii kwamba hajui mumewake juko wapi,pia
analenga kuichochea jamii kwamba anayetuhumiwa kutenda uhalifu akikamatwa
familia yake iandamane,tendo ambalo pia ni kosa la jinai,aidha anatakiwa
kuheshimu haki za watoto na kuacha kuwatumia kama kinga ya kutetea watu
wanaotuhumiwa kutenda uhalifu"alisema Senso.
No comments:
Post a Comment