Mama Lulu na mama wa marehemu Steven Kanumba wanaonekana kuwa karibu
sana siku hizi na hivyo watu kuzidi kuamini kuwa hawana tofauti tena na kusahau
yaliyopita. Dada wa marehemu Steven Kanumba
amejifungua hivi karibuni katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili na mtoto huyo kupewa jina la Steven Kanumba Jr huku mama mzazi wa Elizabeth Michael(Lulu) na mama Kanumba wakiwa na furaha sana, Lulu pia alionyesha furaha yake kwa kuzaliwa mtoto huyo kama picha zinavyoonekana hapo chini. Tunawapongeza tena na tena wazazi hao kwa kuwadhihirishia wanajamii kwa mara nyingine kuwa kila mtu ana amani na mwenzake na hakuna tofauti yoyote kati yao. Mtoto huyo amepewa jina la Kanumba kama ishara ya kumuenzi muigizaji Steven Kanumba aliyekuwa maarufu Afrika mashariki na kuanza kujulikana kimataifa

No comments:
Post a Comment