Taarifa za mwanzo za kusikitisha ambazo
tumezipata hivi punde zinasema mtu mmoja anayedhaniwa kuwa mume au mchumba wa
mwandishi wa habari wa ITV na Radio One Ufoo Saro amefanya mauaji ya kutisha na
yeye mwenyewe kujiua.
Akizungumza na radio one kamanda wa
polisi wa mkoa wa kipolisi wa Kinondoni kamanda Wambura amesema tukio hilo
limetokea majira ya alfajiri ya leo.
Kamanda wambura ameongeza
kuwa mwanaume huyo anafanya kazi Umoja wa Mataifa (UN) huko Sudani ila bado
haijafahamika kwamba anafanyia kitengo gani (japo kwa habari za mtaani zinasema
mtu huyo ni mwanajeshi ila bado hazijathibitishwaKamanda Wambura anasema inasemekana kulikua kuna ugomvi kati ya wawili hao ambapo walishindwa kuelewana na ndipo walipoamua kwenda kwa mama mzazi wa Ufoo Saro (mama mkwe) na ndipo mwanaume huyo alipomshutumu mama mkwe wake kwamba anamtetea mwanae ndipo alipotoa bastola na kumpiga mama yake na Ufoo Saro Risasi ya kichwa na kumuua papo hapo na kisha akampiga Ufoo Saro risasi ya mbili moja ya tumboni na ingine ya mguuni na kudhani kwamba amemuua kumbe amemjeruhi tu kisha kujipiga mwenyewe risasi ya kidevuni na kufariki dunia hapo hapo.
Source: Breaking News - Radio One
No comments:
Post a Comment