Find us on facebook

Pages

Follow Me.

Tuesday, May 21, 2013

MSEVENI AZUNGUMZA KUHUSU MASHOGA.


 Rais wa Uganda Yoweri Museveni, amesema wapenzi wa jinsia moja hawapaswi kuuawa au kudhalilishwa, huku wabunge wa nchi hiyo wakiendelea na mjadala wa kutathmini kuhusu muswada wenye utata wa kupinga wapenzi wa jinsia moja.

Katika matamshi yake ya kwanza hadharani, kuhusu muswada huo, Rais Museveni amekariri kuwa suala la mapenzi ya jinsia moja halipaswi kupewa nafasi kukita mizizi.
Muswada wa awali uliowasilishwa katika bunge la Uganda, ulipendekeza adhabu ya kifo kwa wale watakaopatikana na hatia ya kushiriki mapenzi ya jinsia moja, lakini kipengele hicho kimefutwa katika muswada mpya.
Katiba ya Uganda kwa sasa inaharamisha mapenzi ya jinsia moja.

No comments:

Post a Comment