Find us on facebook

Pages

Follow Me.

Wednesday, June 12, 2013

POLISI KENYA MATATANI KWA MIHADARATI

Mamlaka ya Kitaifa ya kupambana na mihadarati nchini Kenya (NACADA), jamii ya Waislamu, na wakuu wa mashirika ya kijamii nchini humo wameituhumu polisi kuwa
ndiyo inayobariki magendo ya dawa za kulevya na hivyo kukwamisha kampeni mbalimbali za kupambana na tatizo hilo. Mkurugenzi   wa NACADA, Sheikh Juma Ngao ambaye pia amezungumza kwa niaba ya Waislamu amesema kwamba, vita dhidi ya mihadarati haviwezi kufanikiwa iwapo polisi wataendelea kuwakingia kifua mabwanyenye wanaoendesha biashara ya dawa za kulevya. Sheikh Ngao amekanusha madai kwamba NACADA imeshindwa kutekeleza majukumu yake na kusisitiza kuwa, sheria zinapaswa kubadilishwa ili taasisi yake iwe na nguvu zaidi ya kuwachunguza na kuwafikisha mahakamani wale wanaoendesha biashara hiyo haramu. Takwimu zinaonyesha kuwa idadi ya Wakenya wanaotumia dawa za kulevya imepanda katika miaka ya hivi karibuni ikilinganishwa na muongo mmoja uliopita.

No comments:

Post a Comment