Jeshi la polisi limekipiga
marufuku chama cha demokrasia na maendelo(CHADEMA)kufanya shughuli zozote za
kuaga miili ya marehemu kwenye viwanja vya Soweto kwani zoezi la uchunguzi bado
linaendelea kwenye viwanja hivyo .
Akizungumza ofisini kwake kamanda wa polisi mkoani Arusha,
Liberatus Sabas amesema kutokana na uchunguzi unaoendelea wa tukio la bomu
kwenye viwanja hivyo imeonelea kuwa si busara kuweka mkusanyiko wa watu kwani
kutaharibu upelelezi.
Kamanda Sabas amedai kuwa jeshi la polisi liliwataka viongozi wa chama hicho kuwaeleza wafuasi wao mahali sahihi watakapoweza kufanyia shughuli hiyo lakini si kwenye viwanja hivyo.
Hali
kwenye viwanja hivyo imekuwa ya pilika pilika tangu juzi kwa wafuasi wa chama
hicho kujikusanya tokea asubuhi hadi jioni kwa madai ya kuomboleza ..
Hata hivyo viongozi wa chama cha
demokrasia na maendeleo walikaidi agizo hilo na kuanza kujikusanya
uwanjani hapo pamoja na wafuasi wa CHADEMA , hali
iliyoleta mvutano kati ya viongozi wa jeshi la polisi na
wafuasi hao.
Wakati mabishano hayo yakiendelea, Askari Polisi
mmoja alijichanganya na kuingia katikati ya wafuasi wa Chadema pembeni
mwa uwanja huo ambao walikua wanasubiri kujua utaratibu wa kuaga miili ya
Marehemu waliolipuliwa na bomu June 15 2013.
Baada ya hapo,Wafuasi hao hawakupenda kitendo cha Polisi
kujichanganya nao hivyo ikazuka ugomvi huku wakitaka atoke, baada ya dakika
kadhaa mabumu yalianza kusikika.
No comments:
Post a Comment