Na katika habari zilizopo ni kwmba M to the P amereja nchini leo.
Rafiki wa wa karibu wa marehemu Albert
Mangwea aliyekuwa amelazwa nchini Afrika Kusini amerejea Tanzania na yuko
njiani akielekea mkoani Morogoro kwaajili ya kushiriki mazishi ya swahiba wake
Mangwea jioni ya leo (June 6).Akizungumza na Times Fm asubuhi hii Mgaza Pende a.k.a M 2 The P amewashukuru watanzania kwa kumuombea japo hali yake bado haijawa nzuri sana lakini ameamua kurudi Tanzania kuja kumzika ndugu yake Mangwea.
“Ndugu zangu watanzania mimi ni Mgaza Pende M 2 The P nawashukuru sana kwa kuniombea mpaka muda huu, nimeweza kuwasili Tanzania salama na tutakuwa pamoja kwenda kumzika ndugu yangu kipenzi changu Albert Mangwea, nawashukuru sana watanzania kwa kuniombea asanteni na endeleeni kuniombea hali yangu bado haijawa nzuri zaidi, asanteni,”
No comments:
Post a Comment