Find us on facebook

Pages

Follow Me.

Friday, May 17, 2013

VITA YASHIKA KASI NIGERIA.

Operesheni hiyo inakuja baada ya serikali kutangaza hali ya hatari katika majimbo ya Borno, Yobe na Adamawa Kaskazini Mashariki mwa nchi ambako watu 2,000 yatari wameuawa tangu mwaka 2009. Amri ya kutotoka nje kuanzia saa za jioni hadi asubuhi imetangazwa katika jimbo la Adamawa ili kukabiliana na wanamgambo hao. Mwandishi wa BBC katika jimbo la Adamawa anasema kuwa uamuzi huo unashangaza kwani hali ya usalama katika jimbo hilo sio mbaya ikilinganishwa na majimbo ya Borno na Yobe. Mnamo siku ya Alhamisi wanajeshi walivamia kambi za wanamgambo katika mbuga ya wanyama na ambayo inasifika kuwa moja ya ngome kuu za kundi la Boko Haram Msemaji wa jeshi la Nigeria Brigedia Generali Chris Olukolade, alisema kuwa watatumia uwezo wao wote wa kijeshi kukabiliana vilivyo na wapiganaji wa Boko Haram.

No comments:

Post a Comment