Waziri apendekeza Kuanzisha kodi ya zuio ya asilimia 10 ya kamisheni (commission) ya usafirishaji wa fedha kwa njia ya simu za mkononi. Kodi hiyo itakusanywa na kampuni za simu kutoka kwa wakala wanaotoa huduma za kusafirisha fedha kupitia simu za mkononi- Waziri apendekeza Kuongeza kiwango cha Ushuru wa Bidhaa kwenye magari yasiyo ya uzalishaji (Non-Utility Motor Vehicles) ya umri wa zaidi ya miaka 10 kutoka asilimia 20 hadi asilimia 25. Hatua hii inalenga katika kupunguza uagizaji wa magari chakavu, kulinda mazingira na kupunguza ajali
KWA KIFUPI
- Katika kipindi cha Julai hadi Aprili 2013, Serikali ilikopa shilingi bilioni 1,364.7 kutoka soko la ndani la mitaji kwa ajili ya kulipia dhamana za Serikali zilizoiva pamoja na shilingi bilioni 809.1 kwa ajili ya kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo.
- Mwaka 2012/13 Serikali ilikadiria kupata mikopo yenye masharti ya kibiashara shilingi bilioni 1,254.1, sawa na Dola za Kimarekani milioni 800 kwa ajili ya kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo katika bajeti ya mwaka 2012/13 iliyopitishwa na Bunge lako tukufu. Hadi kufikia Mei 2013, Serikali ilipokea shilingi bilioni 947, sawa na dola milioni 600 kutoka benki ya Stanbic, na shilingi bilioni 59.2, sawa na dola milioni 37 kutoka benk ya Credit Suisse.
- Serikali ilikadiria kutumia shilingi bilioni 15,191.9 katika mwaka 2012/13. Mgawanyo wa matumizi ya Serikali katika kipindi hiki ulikuwa kama ifuatavyo: shilingi bilioni 10,597.1 zilitengwa kwa matumizi ya kawaida na shilingi bilioni 4,594.8 zilikadiriwa kutumika kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.
- Hadi kufikia Aprili 2013, matumizi ya kawaida bila kujumuisha malipo ya hatifungani zilizoiva (rollover) yalifikia shilingi bilioni 7,582.6, sawa na asilimia 82 ya makadirio ya mwaka. Kati ya kiasi hicho, malipo ya mishahara ya watumishi wa Serikali, katika wizara, Idara zinazojitegemea, Sekretarieti za Mikoa, Mamlaka ya Serikali za Mitaa na Taasisi za Umma yalikuwa shilingi bilioni 3,209.2 sawa na asilimia 85 ya makadirio ya mwaka ya shilingi bilioni 3,781.1.
- Hadi mwishoni mwa Machi 2013, Deni la Taifa (likijumuisha deni la umma na sekta binafsi) lilikuwa shilingi bilioni 23,673.53 ikilinganishwa na deni la shilingi bilioni 20,276.6 Machi 2012 likiwa ni ongezeko la asilimia 17. Kati ya kiasi hicho, shilingi bilioni 18,282.02 ni deni la nje na shilingi bilioni 5,397.50 ni deni la ndani. Deni la nje, linajumuisha deni la umma la shilingi bilioni 15,203.34 na deni la sekta binafsi ni shilingi bilioni 3,078.69. Kiasi hicho cha deni la nje kinajumuisha deni halisi shilingi bilioni 16,087.43 na malimbikizo ya riba ya shilingi bilioni 2,194.59. Deni la ndani linajumuisha hati fungani za muda mrefu kiasi cha shilingi bilioni 4,261.03 na dhamana za Serikali za muda mfupi kiasi cha shilingi bilioni 1,136.48.
Waziri anapendekeza kufanya marekebisho ya Sheria ya Kodi ya Mapato, SURA 332 kama ifuatavyo: -
(i) Kupunguza kiwango cha chini cha kutoza kodi ya mapato ya ajira kutoka asilimia 14 hadi asilimia 13. Hatua hii inalenga katika kutoa nafuu ya kodi kwa mfanyakazi;
(ii) Kuanzisha kodi ya zuio ya asilimia 10 ya kamisheni (commission) ya usafirishaji wa fedha kwa njia ya simu za mkononi. Kodi hiyo itakusanywa na kampuni za simu kutoka kwa wakala wanaotoa huduma za kusafirisha fedha kupitia simu za mkononi;
(iii) Kutoza kodi ya zuio kwa kiwango cha asilimia 5 kwenye malipo yatokanayo na huduma mbali mbali kama vile huduma za ushauri wa kitaalamu na nyinginezo (Consultancy services and other services). Kodi hii itatozwa bila kujali kama kuna Namba ya Utambulisho wa Mlipa kodi (TIN) au la. Lengo la hatua hii ni kudhibiti na kulinda mapato ya Serikali;
(iv) Kutoza kodi ya zuio kwenye bidhaa zinazonunuliwa na Serikali na Taasisi zake kwa kiwango cha asilimia 2 bila kujali kama kuna Namba ya Utambulisho wa Mlipa kodi (TIN) au la. Lengo la hatua hii ni kudhibiti na kulinda mapato ya Serikali;
(v) Kufuta msamaha wa kodi ya zuio kwenye ukodishaji wa ndege kwa walipa kodi wasio wakazi (non-resident). Hatua hii inalenga katika kupunguza misamaha ya kodi na kuhuisha mapato ya Serikali;
Hatua hizi za Kodi ya Mapato kwa pamoja zitaongeza mapato ya Serikali kwa kiasi cha shilingi milioni 131,686.
Waziri anapendekeza kufanya marekebisho katika Sheria ya Ushuru wa Bidhaa, SURA 147 kama ifuatavyo:-
(i) Kuongeza kiwango cha Ushuru wa Bidhaa kwenye magari yasiyo ya uzalishaji (Non-Utility Motor Vehicles) ya umri wa zaidi ya miaka 10 kutoka asilimia 20 hadi asilimia 25. Hatua hii inalenga katika kupunguza uagizaji wa magari chakavu, kulinda mazingira na kupunguza ajali;
(ii) Kuanzisha kiwango kipya cha Ushuru wa Bidhaa cha asilimia 5 kwenye magari ya uzalishaji (Utility Motor Vehicles) yenye umri wa zaidi ya miaka 10 yanayotambuliwa katika HS Code 87.01, 87.02 na 87.04. Hatua hii haitahusisha magari chini ya HS Code 8701.10.00; na HS Code 8701.90.00 ambayo kimsingi ni matrekta yaliyounganishwa; na magari yasiyounganishwa chini ya HS Code 8702.10.11; 8702.10.21, 8702.10.91; 9702.90.11, 8702.90.21; 8702.90.91; HS Code 87.04; 8704.10.10; 8704.21.10; 8704.22.10; 8704.23.10; 8704.31.10, na 8704.32.10, 8704.90.10. Lengo la kuanzisha kiwango kipya cha ushuru ni kupunguza uagizaji wa magari chakavu, kulinda mazingira na kupunguza ajali. Aidha, matrekta na magari yasiyounganishwa hayatatozwa ushuru huu kwa nia ya kuhamasisha uwekezaji kwenye sekta ya uunganishaji wa magari na hivyo kuongeza ajira na mapato ya serikali;
(iii) Kurekebisha viwango vya Ushuru wa bidhaa kwenye mafuta ya Petroli kama ifuatavyo: -
a] Mafuta ya Dizeli kutoka kiwango cha sasa cha shilingi 215 kwa lita hadi shilingi 217 kwa lita ikiwa ni ongezeko la shilingi 2 tu;
b] mafuta ya Petroli kutoka kiwango cha sasa cha shilingi 339 kwa lita hadi shilingi 400 kwa lita; na,
c] mafuta ya Taa kiwango hakitabadilika kwa kiwango cha sasa

No comments:
Post a Comment