ZITTO ATOA KAULI NZITO.
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Zitto Kabwe amesema Serikali inakosa Dola 885. milioni za Marekani (Sh 1.5trilioni) kutokana na kampuni za madini kukwepa kodi.
Akihutubia mkutano wa hadhara huko Shelui mkoani Singida jana, Zitto alizituhumu kampuni hizo kuwa zinatumia mwanya wa kutoa mchanganuo wa manunuzi, ambayo si ya kweli ili kukwepa kodi.
Zitto, ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, alisema ripoti ya Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA), inaonyesha kuwa Serikali imekuwa ikipunjwa kodi yake kutokana na mwanya wa manunuzi unaotumiwa na kampuni za madini.
Alisema TMAA ilikagua kampuni 14 mwaka jana na kugundua kuwa Serikali ilikosa kiasi cha Sh 425 bilioni kutokana na ukwepaji kodi.
Alisema mabilioni hayo inayopotea yangeweza kusaidia katika sekta ambazo hazifanyi vizuri katika maandeleo.
“Hii ni hujuma kubwa kwa kitaifa, kwa kweli hatupaswi kuachia mambo haya, Serikali inapaswa kushughulikia suala hili,”
alisema Zitto.
Amemtaka Waziri wa Fedha na Uchumi, Dk William Mgimwa, kushughulikia suala hilo kwani sekta ya madini inapaswa kuwa chachu ya maendeleo ya nchi.
Kwa upande wake Dk Mgimwa alisema Serikali inatazama upya mikataba ya madini, ili kujiridhisha kuona kama inakidhi mahitaji ya taifa.
Pia alisema wataifanyia kazi kikamilifu ripoti ya wakaguzi wa madini.
CHANZO.MWANANCHI
No comments:
Post a Comment