Find us on facebook

Pages

Follow Me.

Tuesday, June 11, 2013

LWAKATARE APEWA DHAMANA.


Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Wilfred Lwakatare na mwenzake Joseph Ludovick Rwezaura, lhivi punde wamepata dhamana na endapo
atatimiza masharti ya dhamana leo atakuwa nje.

Taarifa za awali zimebainisha kwamba dhamana ya Lwakatare iko wazi na ataachiwa huru baada ya kutimiza masharti yafuatayo.

Masharti hayo ni kuwasilisha mahakamani hati yake ya kusafiria, kuwa na wadhamini wawili na kulipa bondi ya Sh10 milioni. Hivi sasa katika mahakama hiyo nyaraka kutoka ofisi za serika za mitaa zinahakikiwa na maofisa wa mahakama.

Kutokana na hali hiyo mpaka sasa Lwakatare na mwenzake hawajaachiwa huru ila wanatajiwa kuachiwa huru  eo saa 8:00 mchana endapo watakamilisha masharti hayo.

Washtakiwa hao jana walikwama kupata dhamana na hakimu aliahidi kutoa dhamana leo saa 2:00 asubuhi.  Kutokana na maelezo ya Hakimu leo ametekeleza ahadi yake isopokuwa masharti ya Mahakama ya Hakimu Mkazi  Kisutu ndio yamekwamisha.

Awali Lwakatare na mwenzake walikuwa wameshtakiwa kwa kosa la ugaidi na kula njama na kumteka Mhariri wa Mwananchi Dennis Msacky, lakini Mahakama Kuu iliwafutia mashtaka ya ugaidi na kubaki na shtaka la kula njama.

No comments:

Post a Comment