Mhadhiri wa chuo kikuu
cha
Delta State huko nchini Nigeria alijikuta katika aibu kubwa baada ya
kuvuliwa nguo na kubaki uchi wa mnyama baada ya mwanafunzi wa kike aliyekuwa
akisumbuliwa na Mhadhiri huyo kuamua kumfanyia umafia kwa kumuwekea mtego.
Hatua ya kudharirishwa
kwa Mhadhiri huyo ilikuja baada ya mwalimu huyo kumtishia Tega na kumwambia
kuwa atamferisha kama hata kubali kufanyanae mapenzi.Kabla ya hapo Mhadhiri
huyo aliwahi kumtongoza mwanafunzi huyo lakini mwanafunzi huyo alimkatalia kata
kata baada ya kuona hivyo Mhadhiri huyo aliamua kutumia wadhifa alionao kwa
kumtishia kuwa kama hato kubali kulala nae basi atamfelisha mtihani.
Baada ya kuona hivyo
Tega aliamua kumkubalia Mhadhiri huyo na kumshawishi badala kwenda kwenye
hoteli kuchukua chumba ni bora waende nyumbani alikopanga mwanafunzi huyo ili
wapunguze gharama,kuona hivyo Mhadhiri huyo alikubali haraka na kwenda nyumbani
kwa Tega bila kujua kuwa kuna mtego amewekewa kumbe kabla ya hapo Tega alikuwa
amesha waambia majirani zake na wanafunzi wenzake kuwa atahakikisha anamrubuni
Mhadhiri huyo mpaka akubali kuvua nguo akisha kubali tu anamuaga kuwa anakwenda
chooni kisha anawapigia simu waje kumuumbua Mhadhiri huyo kwani milango yote
alikuwa ameirudishia tu na alikuwa ameshawaelekeza chumba ambacho atakuwepo
Mhadhiri huyo.
Basi baada ya kuwapigia majirani na wanafunzi wenzake walifika eneo hilo la tukio na kufungua milango kimya kimya na kufanikiwa kuingia ndani mpaka chumba alipo Mhadhiri huyo ndipo walipo fanikiwa kumkuta Mhadhiri huyo akiwa uchi wa mnyama kitandani na kisha kumtoa nnje na kumtembeza uraiani ili watu wajionee wenyewe nini baadhi ya wahadhiri hufanya kwa wanafunzi wa kike.

No comments:
Post a Comment