Rasimu ya katiba imeziduliwa leo hii amabapo maswala mbalimbali yameibuka likiwemo la Mgombea binafsi kupendekezwa kuwepo katika katiba ijayo
Suara zima la muungano limependekezwa kuwa la serikali tatu.hivyo basi kuwepo na bunge la muungano Itakuwepo serikali ya shirikisho,serikali ya tanzania bara,na serikali ya mapinduzi.Na mambo ya muungano yapunguzwe kutoka 22 mpaka 7 amabayo ni yafuatayo
KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO
ULINZI NA USALAMA.
URAIA NA UHAMIAJI
SARAFU NA BENKI KUU.
MAMBO YA NJE
USAJILI WA VYAMA VYA SIASA.
USHURU WA BIDHAA PAMOJA NA MAPATO YASIYO YA KODI YANAYOTOKANA NA MAMBO YA MUUNGANO.
Tume imependekezaUmri wa mgombea urasisi kuwa miaka 40
Pia tume imependekeza kwamba kiwango cha kula sasa kuwa na asilimia 50 asipofikisha duru ya pili itafanywa
Tume imependekeza kuwa matokeo ya uchaguzi ya Raisi kuhojiwa mahakamani na si mwingine wakuhoji bali ni mgombea uraisi tu'
Kuhusu Madaraka ya Raisi :Raisi atabaki na madaraka yake ya uteuzi.Jaji mkuu mawaziri wakuu wtadhibitishwa na bunge,kwa viongozi wa ulinzi na usalama raisi atawateua kutokana na mapendekezo ya baraza la ulinzi na usalama.
Kuhusu kinga ya Raisi tume imependekeza kwamba kinga ya Raisi Ibaki.
Tume imependekeza ukomo wa vipindi vitatu vya kuwa bunge,vilevile wanachi wawe na mamlaka ya kumuondoa mbunge,na kusiwepo na uchaguzi mdogo ikitokea nafasi itajazwa na chama husika kilichokuwa kimeshinda isipokuwa kama mbunge alikuwa mbunge huru utakuwepo uchaguzi mdogo.
Tume imependekeza kuwepo mahakama ya juu (supreme court)
PIA TUME IMEYAKATAA MASWALA YA
SERIKALI ZA MAJIMBO NA KUSEMA KWAMBA YATAGAWA NCHI KATIKA UDINI UKABILA PAMOJA NA UKANDA.
SUALA ZIMA LA MAHAKAMA YA KADHI Tume imesema kuwa suala hilo linaweza kuwepo japo halimo katika mapendekezo ya tume,imesema kwamba hili sio swala la muungano kwa hiyo nchi husika itashugulikia swala hilo.Wamesema swala hili kwa upande wa bara wanaweza kuchukua uzoefu wa zanzibar hivo basi suala la kuwepo kwa mahakama ya kadhi au kutokuwepo wanawaachia nchi husika.
Imeandikwa na
MBARAKA KATELA
No comments:
Post a Comment