Baada ya Mh.Mwigulu Nchemba kufichua namna CHADEMA walivyomuandaa video cameraman wa kurekodi tukio zima la bomu arusha.
Chadema wamekuja na
DVR na CCTV.Kwanini wamekuja na kauli hii baada ya mwigulu? Ni wazi Mh.mwigulu ametegea mbinu yao ndogo sana sasa wamechanganyikiwa. Mitambo ya DVR na CCTV huwa haizunguki kuchukua tukio ina focal point moja tu.
DVR ya chadema inamikono inazunguka waliko watu,ikaona bomu ikalifuata lilipotua,ikamkimbilia mbowe alipo..ikarudi kwenye damu.
Uongo mliumbiwa
MH:MWIGULU NCHEMBA ALIPUA MTEGO WA CHADEMA WA KUMUANDAA VIDEO CAMERAMAN ALIYECHUKUA VIDEO YA MLIPUKO WA BOMU LA ARUSHA, CHADEMA WAHAHA KUJINASUA WAKIMBILIA KUTAJA CAMERA ZA DVR NA CCTV.
Kila mmoja wetu amesikitishwa sana na namna tukio la mlipuko wa bomu kwenye mkutano wa chadema pale Arusha ulivyotokea na kuangamiza maisha ya ndugu zetu wasio na hatia. Hili si tukio la kulichekea,si tukio la kufurahia,si tukio la kusherekea,si tukio la kugongeana glasi kwamba tumewaweza uchaguzi sasa umeahirishwa.
Hili ni tukio la kukemea kwa nguvu moja,ni tukio la kusaka mtekelezaji wa unyama huu kwa udi na uvumba.Ni tukio la kusikitisha kwa kila mmoja wetu,ni tukio la kinyama. Kutokana na mlipuko huo,maelfu na maelfu (malaki)ya watanzania waliobahatika kupita mitandaoni na hata kusikia kisa kilivyo na danadana zinavyopigwa na viongozi wa chadema,moja kwa moja utakuta sehemu kubwa ya watanzania wananyoosha vidole vyao moja kwa moja kwa chadema kuhusika na tukio zima la mlipuko wa bomu tena kwa kupanga. Serikali ya Tanzania kimsingi katika jambo lolote lile ni lazima ilaumiwe,ni lazima ilaumiwe kwa sababu ndiye baba na mama wa watanzania.
Hata mtu aliyeamua kulala nyumbani bila kujishughulisha kutafuta kazi akibanwa na njaa atailalamikia serikali anasahau kuwa yeye anawajibu wa kuamka na kwenda kutafuta riziki. Kwamaana hiyo serikali kulalamikiwa na chama tawala kulalamikiwa ni jambo la lazima na ni kawaida katika nchi yoyote,unataka ukamlalamikie nani?.Katika hili hata mungu angekuwa ndiye serikali lazima watanzania tungemlalamikia kwa sababu ndiye kichwa,ndiye baba,ndiye mama wa maisha yetu.
Baada ya bomu la Arusha wote tumekuwa mashuhuda kuwa viongozi wa CHADEMA wamekuwa wakwanza kujitokeza na kusema wanaushahidi wa video (hii hapa) na risasi zilizotumika wanazo. Baada ya kuachia video yao (CHADEMA) ambayo wameiita part one kwa maana kwamba kuna part Two. Video yao ya kwanza tu imewahukumu moja kwa moja kuwa wao ni washukiwa namba moja wa mlipuko wa bomu pale kwenye mkutano wao.
Video waliyoiweka mtandaoni kupitia kijana wao Ben saanane utakuta aliyekuwa anachukua tukio lile kabla na baada ya mlipuko wala hakushituka kuwa kuna bomu limelipuka eneo hilo,yeye aliendelea kushuti na kusogelea sehemu lilipotua bomu..zaidi akaenda walipo akaina mbowe na Lema(ameshikilia boksi la fedha) baadae anayeshuti video anarejesha video hadi kwenye eneo damu zilipotapakaa n.k Moja kwa moja video inatuonesha kuwa aliyekuwa anachukua video ile ni binadamu kama mimi na sio kitu chochote kile kama chadema wanavyotaka kupotosha umma kuwa eti walifunga mitambo Baada ya kuachia video hiyo,
MH: MWIGULU LAMECK NCHEMBA MADELU aliyefichua ugaidi wa CHADEMA kwa watanzania na waandishi wa habari mapema mwaka huu na kupelekea Mkuu wa Usalama wa CHADEMA Wilfred Lwakatare kunasa kwenye mtego huo na kupandisha kizimbani. Kama kawaida ya Mwigulu akaibua hoja nzito(jiwe) kuwa video waliyoiweka CHADEMA na kuisambaza mitandaoni eti ndio ushahidi ni video ambayo aliyekuwa anachukua alikuwaamepangwa na nikama alikuwa nashuti sendoff yaani wala hashituki kuwa kuna bomu limelipuka.Watanzania wapi na wapi bomu linalipuka hapa wala mtu hashituki? Hii kauli ya Mh:Mwigulu Nchemba ilikuwa kama mwiba,yaani chuma kizito kimeanguka juu ya utosi wa CHADEMA.
Ndipo Mh:Mbowe na vijana wake wakaitana na kuweka kikao,kwenye maazimio hayo wakasema tuwambie watanzania ile video ilichukuliwa na mtambo maalumu wa camera za DVR na CCTV. DVR na CCTV ni camera zinazofungwa eneo flani kwa lengo la kunasa tukio husika la eneo hilo.Yaani camera hizo zinanasa kitu chochote bila kuchambua,zinanasa hata panya aliyekatiza eneo hilo. Mapungufu ya CAMERA hizi zenyewe hazizunguki kuchukua tukio eneo flani na flani.
Yanii ulipoitegesha ichukue ni hapo hapo,huwezi kuta imezunguka ikachukua na sehemu nyingine.Ndio maana wanaofunga cctv au dvr camera hawafungi moja wanafunga nyingi maeneo tofautitofauti ilikusaidia angalau kupata matukio ya eneo lote lakini si kwa kuspecify kwamba itachukua huyu na kumwacha huyu. Camera zitazunguka kunasa matukio mengine endapo binadamu ameishika anaizungusha.Zinauwezo wa kunasa umbali mrefu na karibu na zinaweza kuwekwa kwenye engo ya nyuzi mia tatu sitini,180 au 90.Inategemeana na ukubwa wa camera.
SASA CHADEMA WAKASEMA WAMETUMIA DVR NA CCTV, HII NI KUJIDHALILISHA SANA KWA KIWANGO CHA HALI YA JUU SANA.
CAMERA gani ya DVR au CCTV inashuti video kwa mtindo huu.Yaani ianaaza kuonesha watu wanavyoimbaaa weeee,inazunguka kuonesha eneo la jukwaaa…Camera hiyo inashituka kuwa kuna bomu limelipuka eneo hilo inalifuata bomu lilipotua then inaanza kuonesha namna majeruhi walivyoathirika,camera hiyo ya DVR inakwenda mbali zaidi na kuacha watu wote inawafuata Mbowe na lema waliposimama inawaonesha kwa muda wa dakika 3,hiyo camera ya DVR ya chadema inatambua lema ameshika boksi la hela inalionesha..baadae inarejea walipo lala Marehemu nakuanza kuonesha damu zilivyomwagika,hiyo hiyo DVR ya chadema anaamua kuchukua watu wanaobeba waathirika wa bomu.Mwisho inamalizika na kurejea jukwaani.
Duhhh watanzania wenzangu hao ndio CHADEMA na mitambo ya DVR NA CCTV kweli wamejidhalilisha kupita kiasi. Katika hili CHADEMA hamnapakutokea mkili tu mlipanga mlipuko na makaanda watu wa kushuti video ya tukio hilo ili mpate kuwapelekea uingereza na taasisi zingine zinazowapatia fedha.
PART TO YA CHADEMA KWENYE VIDEO WANAYOIANDAA MUADA HUU AKINA BEN SAANANE NA MZEE MWANAKIJIJI(Mwanakijiji ndiye anayeandaa uchakachuzi wa video hiyo nchini marekani)
Nadhani baada ya kuona critism hii ya Mh:Mwigulu nchemba watajitahidi kutingisha tingisha video ili aliyekuwa nashuti aonekane alishituka. PIa wanaweza kuacha kabia kutaja CAMERA za DVR na CCTV kwa sababu zimewaumbua tayari kwamba wamezikabizi kazi ambayo camera hizo hazinauwezo wa kuifanya(Kuzunguka na kuchukua wahusika flani flani(mbowe,lema,lilipotua bomu,boksi la fedha,damu n.k)). Video ya pili inaonesha askari akifyatua risasi kama walivyotangulia kusema,Huku mtu aliyevalia jinsi ya blue anakimbia kuelekea kwenye gari.
Hivyo DVR ya chadema inafuatilia mtu anavyokimbia hadi anaingia kwenye gari na ianaokota mabaki ya risasi na kumpelekea mbowe. Ukweli ni kwamba mtu anayeonekana askari kwenye hiyo video ni mmoja wa kijana wa mbowe(Mh;Mbowe amefadhili ununuzi wa mavazi ya FFU yanayofanana kabisa kabisa na FFU halisi).Ndio maana Mbowe aliongoza kufukuza askari wasisogelee mkutano wako,kwa sababu alijua askari feki akikutana na askari halisi dili yake itabumbuluka. Hivyo askari na anayekimbia na anayerusha risasi ni vijana wa Mh:Mbowe.Ni vijana walioandaliwa na CHADEMA na mafunzo yao yamefanyikia hapo Kenya.
No comments:
Post a Comment