Watu wawili wanahofiwa kupoteza maisha
na wengine
wengi kujeruhiwa kutokana na mlipuko wa bomu lililolipuka kwenye mkutano wa CHADEMA katika eneo la Soweto, kata ya Kaloleni jijini Arusha, wakati wa kufunga kampeni za uchaguzi wa madiwani katika maeneo ya jiji hilo.
Waliojeruhiwa wamekimbizwa katika
hospitali za Seliani na Mount Meru ambapo baadhi ya watu waliojitolea
wanashirikiana na Madaktari na Wauguzi wa hospitali hizo kutoa huduma ya
kwanza.
Bomu hilo linaelezwa kuwa lilitupwa kwenye mkusanyiko wa watu, lilipuka mwendo wa saa kumi na mbili na robo jioni wakati mkutano huo ulipokuwa umekwisha na shughuli ya kukusanya michango ikiendelea.
Viongozi wa juu wa CHADEMA, Freeman Mbowe na Godbless Lema walikuwepo na wameendelea kuwepo kwenye eneo baada ya mlipuko huo.
wengi kujeruhiwa kutokana na mlipuko wa bomu lililolipuka kwenye mkutano wa CHADEMA katika eneo la Soweto, kata ya Kaloleni jijini Arusha, wakati wa kufunga kampeni za uchaguzi wa madiwani katika maeneo ya jiji hilo.
Kamanda wa polisi mkoani humo, Liberatus Sabas yupo katika moja ya hospitali
hizo.
Bomu hilo linaelezwa kuwa lilitupwa kwenye mkusanyiko wa watu, lilipuka mwendo wa saa kumi na mbili na robo jioni wakati mkutano huo ulipokuwa umekwisha na shughuli ya kukusanya michango ikiendelea.
Viongozi wa juu wa CHADEMA, Freeman Mbowe na Godbless Lema walikuwepo na wameendelea kuwepo kwenye eneo baada ya mlipuko huo.
No comments:
Post a Comment