Find us on facebook

Pages

Follow Me.

Wednesday, May 22, 2013

MTWARA KWACHAFUKA TENA.

Mabomu  maeneo ya Magomeni-Mtwara yanaendelea kurindima. Sasa hali si shwari kila eneo, Mabavu yamechukua mkondo wake. Wananchi wamejifungia majumbani mwao. Chuki dhidi ya Polisi yaimarika. Polisi wanapiga mabomu bila mwelekeo. Magomeni na sokoni kimenuka, mabomu yanarushwa na wananchi wanakimbia ovyo

Waziri wa Nishati amesoma hotuba yake kwa hisia kali na mbwembwe. Mwishoni amesema bomba la gesi linajengwa kutoka Mtwara kwenda Dar. 

Maduka yote yamefungwa, baa zimefungwa, hakuna huduma za usafiri, ofisi za serikali zimepwaya kimsingi hakuna lolote linalofanyika
 Boda boda zinazoonekana maeneo ya Nkanaledi na abiria zinapigwa mawe. 
Makachero nao wanajifanya madereva wa boda boda na Bajaji, Tax wengine wanatembea na magari ya Serikali.
 
Maeneo yote yametawaliwa na ukimya.

No comments:

Post a Comment