Find us on facebook

Pages

Follow Me.

Wednesday, May 22, 2013

TUME YAPENDEKEZA WAKUBWA KUSHTAKIWA KENYA.


Rais wa Kenya  Uhuru Kenyata na naibu wake wametajwa katika ripoti inayowahusisha na ghasia za baada ya uchaguzi katika ripoti hiyo iliyosubiriwa kwa muda mrefu kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu.Ripoti hiyo hata hivyo haikutoa mapendekezo ya hatua za
kuchukuliwa dhidi ya Rais Kenyatta na naibu wake William Ruto.Rais Kenyatta na bwana Ruto wanakana tuhuma hizo.Mwenyekiti wa tume hiyo, aliambia BBC kuwa ni kwa sababu wawili hao wanakabiliwa na kesi ya uhalifu dhidi ya binadamu katika mahakama ya kimataifa ya ICC.
Tume ya maridhiano na haki ilikabidhiwa jukumu la kuchunguza visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu vilivyofanywa tangu mwaka 1963 nchi hiyo ilipojipatia uhuru wake.
Iliundwa baada ya ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2007/08 uliozua ghasia miaka mitano iliyopita kama njia ya kuleta maridhiano miongoni mwa wakenya.
Baada ya uchaguzi huo, watu 1,500 waliuawa na wengine zaidi ya 600,000 kulazimika kutoroka makwao.
Kenyatta na Ruto, waliokuwa mahasimu katika uchaguzi wa mwaka 2007, walishinda uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi Machi baada ua kuungana chini ya muungano wa Jubilee.
Licha ya kuwa hakuna mapendekezo yaliyotolewa na tume hiyo dhidi ya Rais na naibu wake, inapendekeza uchunguzi zaidi dhidi ya maafisa wakuu waliotajwa kuhusika na ghasia za baada ya uchaguzi mwaka 2007 na hata kufunguliwa mashtaka
Baadhi ya waliotajwa ni pamoja na waziri mpya wa madini Najib Balala na maseneta wawili.
Hata hivyo yume hiyo ilimtaka rais Kenyatta kuwaomba radhi wakenya kwa makosa waliyotendewa chini ya seri9kali zilizopita katika kipindi cha miezi sita tangu kukabidhiwa ripoti hiyo hapo jana.
Rais mstaafu Daniel Moi pia alitajwa katika ripoti hiyo akihusishwa na mauaji ya waliokuwa wanasiasa mashuhuri wakati wa utawala wake

No comments:

Post a Comment