Msemaji wa kundi hilo, amesema kuwa makabiliano hayo yalifanyika umbali wa kilomita 12 Kaskazini mwa Goma, nalo jeshi la serikali pia limeitikia kuwa makabliano yalitokea usiku wa kumakia leo ingawa haijathibitishwa ikiwa kulikuwa na majeruhi.
Duru zinasema kuwa waasi hao walikuwa wametishia jeshi la serikali kwa muda wa wiki moja kabla ya kufanya mashambulizi leo.
Mwandish wa BBC mjini Goma, Jonathan Kachelewa ameambia BBC , kuwa msemaji wa jeshi la serikali aliyeongea naye alisema waasi walianza kushambulia vituo vya jeshi katika eneo hilo, na kuwa mapigano yamekuwa yakiendelea tangu saa tisa usiku wa kuamkia leo.
Kulingana na Kachelewa, duru zinatofautiana kuhusu nani aliyeanza mapigano au nini chanzo cha mapigano yenyewe kwani waasi wanasema kuwa wao ndio walianza kushambuliwa
Familia nyingi zimeachwa bila makao kufuatia vurugu linalosababishwa na M23
Pia yametokea huku kikosi cha kwanza cha wanajeshi wa UN kikitarajiwa kuwasili mwezi huu katika juhudi za kupambana na waasi hao.
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, anatarajiwa kuzuru DRC Jumatano kama sehemu ya ziara yake ambapo atatembelea Goma , Kigali Rwanda na Entebbe Uganda.
Waasi hao waliuteka mji wa Goma, Novemba mwaka jana lakini wakaondoka siku kumi baadaye baada ya kuahidiwa mazungumzo na serikali ya DRC. Lakini tangu kuondoka wamekuwa wakiyateka baadhi ya maeneo karibu na mji huo
Waasi hao inadaiwa wanaungwa mkono na nchi jirani ikiwemo Rwanda na Uganda. Hata hivyo nchi hizo zimekanusha madai hayo.
No comments:
Post a Comment