Watekaji nyara Kusini mwa Yemen, wamewaachilia wafanyakazi watatu wa
shirika la Msalaba mwekundu pamoja na mkalimani wao mwenye uraia wa
Yemen.Wafanyakazi hao wa kigeni, raia wa Uswizi, Mkenya na Mmisri, walitekwa nyara siku ya Jumatatu mjini Jaar katika mkoa wa Abyan.
Kuachiliwa kwa watatu hao kunakuja baada ya viongozi wa kijamii kuwaomba watekaji nyara hao kuwaachilia.
Visa vya utekaji nyara wa wafanyakazi wa kigeni, ni kawaida kutokea nchini Yemen.
Watu kutoka makabila fulani wanasifika kwa kuwateka watu nyara kwa lengo la kutaka serikali kuwashughulikia malalamiko yao.
Lakini wapiganaji kutoka kundi la kigaidi la al-Qaeda, pia wamekuwa wakidai kutekeleza baadhi ya visa hivyo.
Mapema mwezi huu, wanandoa wawili kutoka Finland
walitekwa nyara mwezi Disemba na kisha kuachiliwa. Mnamo mwezi Februari
mwalimu mwenye uraia wa Uswizi aliachiliwa na watekaji nyara baada ya
kuzuiliwa kwa zaidi ya mwaka mmoja.
No comments:
Post a Comment