Polisi nchini Ugandan wamevamia ofisi za magazeti kufuatia taarifa
kwamba Rais Yeweri Museveni anamuandaa mwanawe wa kiume kumrithi urais.
ituo viwili vya Redio pia vamiwa na kuzimwa , hii ni kwa muujibu wa gazeti la serikali la New Vision.
Wiki iliyopita magazeti ya Uganda
yalidai kuwa kuna njama za kuwaua wale watakao pinga mpango wa Rais
Museveni kumuandaa mwanawe kuchukua madaraka ya Uganda.
Magazeti hayo yalidai kuwa mipango hiyo ya mauaji yalitolewa na Mkuu fulani wa jeshi la Uganda.
Bwana Museveni, ambaye amekuwa madarakani tangu 1986, anatarajiwa kung'atuka uongozini mwaka 2016.
Kwa muda mrefu kumekuwa na madai kwamba Museveni
anamuandaa mwanawe Muhoozi Kainerugaba,ambaye ni brigadier jeshini
kushikilia uongozi wa Uganda.
Lakini serikali ya Museveni imekanusha kwamba kuna mipango kama hiyo.
Ofisi za Gaeti la Daily Monitor zilizovamiwa na polisi wa Uganda.
No comments:
Post a Comment