Polisi katika mji mkuu wa Tunisia, Tunis, wametumia moshi wa kutoza machozi dhidi ya waandamanaji waliokuwa wakirusha mawe.Waandamanaji hao ni wa chama cha Waislamu wa msimamo mkali, Ansar
al-Sharia, ambao wakijaribu kufanya mkutano wa hadhara uliopigwa
marufuku.
Jumatano chama tawala cha Waislamu wa msimamo wa
wastani, Ennahda, kilisema mkutano mkuu wa Ansar al Sharia umepigwa
marufuku kwa sababu kundi hilo halikupata kibali.
Lakini Ansar al Sharia iliahidi kusonga mbele na mkutano.
No comments:
Post a Comment