Find us on facebook

Pages

Follow Me.

Tuesday, May 21, 2013

WASICHANA WATATU NA MAMA YAO WABAKWA NIGERIA.

Katika hali isiyo ya kawaida Nchini Nigeria wasichana watatu pamoja na mama yao wamebakwa wakati huo wakiwa wanatishiwa kwa bunduki.

MSEVENI AZUNGUMZA KUHUSU MASHOGA.


 Rais wa Uganda Yoweri Museveni, amesema wapenzi wa jinsia moja hawapaswi kuuawa au kudhalilishwa, huku wabunge wa nchi hiyo wakiendelea na mjadala wa kutathmini kuhusu muswada wenye utata wa kupinga wapenzi wa jinsia moja.

KUMBUKUMBU YA KUZAMA KWA MELI YA MV.BUKOBA

 Mnamo tarehe kama ya leo Mei 21 mwka 1996 meli ya Mv Bukoba ikiwa imebakiza km tkribani 54

Monday, May 20, 2013

HII NDIO RASIMU YA SERA YA GESI.

Kama hujaweza kuiona rasimu ya sera ya gesi chukua mda wako kwa kuisoma hapa chini

POLISI WAVAMIA KITUO CHA MAGAZETI UGANDA.

 Polisi nchini Ugandan wamevamia ofisi za magazeti kufuatia taarifa kwamba Rais Yeweri Museveni anamuandaa mwanawe wa kiume kumrithi urais.

BREAKING NEWS; MHESHIMIWA MBOLINYI AZIMIWA KIPAZA SAUTI BUNGENI.

Katika hali isiyo ya kawaida mda huu mheshimiwa Mbilinyi akiwa anaanza kusoma hotuba yake kipaza sauti kilizimwa na hiyo ni

BABA YAKE GARRY NEVILLE MATATANI.

 Baba yake mwanasoka  Garry Neville anashutumiwa kwa kosa la unyanyasji wa kijinsia.

PICHA; MHESHIMIWA ZITTO AKIONGEA KATIKA TAWI LILIROFUNGULWA JUMAMOSI.


PICTURE OF THE DAY.


WAFANYAKAZI RED CROSS WAACHIWA BAADA YA KUTEKWA NYARA.

Watekaji nyara Kusini mwa Yemen, wamewaachilia wafanyakazi watatu wa shirika la Msalaba mwekundu pamoja na mkalimani wao mwenye uraia wa Yemen.

MAANDAMANO YAZIMWA TUNISI.

Polisi katika mji mkuu wa Tunisia, Tunis, wametumia moshi wa kutoza machozi dhidi ya waandamanaji waliokuwa wakirusha mawe.

DRC KWAWAKA MOTO

Waasi wa kundi la M23 Kaskazini mwa Goma, Mashariki mwa DRC wamekuwa wakipigana na majeshi ya serikali usiku wa kuamkia leo (jumatatu). Mapigano hayo yametokea katika eneo ambalo waasi wameteka tangu Novemba mwaka jana.

MSIGWA ALIVYOWASILI MAHAKAMANI LEO.

 Wananchi wakiwa nje ya MAHAKAMA walpozuiliwa kutoingia ndani ya Mahakama kipindi Mbunge wao alipo wasili mahakamani hapo.

MAZISHI KUHUSU CHINUA ACHEBE.

Mazishi ya mwandishi maarufu wa riwaya wa Nigeria, Chinua Achebe, yameanza katika mji wa Ogidi, kusini-mashariki mwa nchi ambako ndiko alikotoka.

MANENO YA RAIS KAGAME KUHUSU VIKOSI VYA UN DRC

Rais wa Rwanda Paul Kagame alitoa mtazamo mkali wa ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa mataifa ulioko katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

PICTURE OF THE DAY.


MAJAMBAZI WATIWA MBARONI NA KUUAWA.

Watu wawili kati ya watatu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wameuawa kwa kupigwa risasi na polisi jijini Mwanza baada ya kuvamia duka linalouza bia za jumla iliyopo eneo la Igoma na kwa nia ya kutaka kupora fedha za mauzo

Sunday, May 19, 2013

DIAMOND NA NEY WAFUNIKA DAR LIVE

  Wasinii wawili Nchini Diamond na Ney wa Mitego wkiwa jukwaani Dar Live wakati wa uzinduzi wa wimbo wa muziki gani

INAKUHUSU.

PICHA ZA CCM WAKIWA DODOMA LEO.

 wajumbe wakiwa kwenye mkutano wanamsikiliza mwenyekiti wao wa chama Jakaya Mrisho Kikwete.
 Mh Mwiguru Nchemba akiteta jambo na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar) Vuai Ali Vuai na Katibu wa NEC Oganaizesheni Dk. Muhammed Seif Khatib kwenye kikao hicho.

POLISI KENYA WAWAUA WASHUKIWA WAWILI.

Polisi mjini Nairobi, Kenya, wamewapiga risasi na kuwauwa watu wawili - mwanamume na mwanamke - baada ya watu hao kurusha maguruneti mane na kuwajeruhi askari kama watano.

MSIGWA MBARONI


Baada ya fujo zilizotokea mjini IRINGA sasa kwa habari ambazo bado hazijadhibitishwa rasni Mbunge huyo anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kuwaongoza wananchi kufanya fujo hizo.

MTANDAO WA KENYA WAMWAGA MBARIKA LIST YA ILLUMINATI NJE WATANZANIA WAMO.








PROF JAY AFUNGUKA.

Msanii Maarufu nchini PROF JAY amefunguka juu ya bifu linaondelea kati ya mwanadada lady jaydee na clouds FM.Msanii huyo ameyasema hayo katika FUNGUKA NA RISASI.

PICTURE OF THE DAY.

HII INAKUHUSU WEWE MFANYABIASHARA AMBAE UNAWEZA KUONYESHA BIDHAA ZAKO KWA NJIA HII.


VURUNGU ZATANDA MJINI IRINGA.

CHEKA NA MUBAAH.


SOMA HAPA ALICHOKIONGEA HALIMA MDEE KUHUSU USAGAJI.

Saturday, May 18, 2013

CHEKA NA MUBAAH.



ANACONDA TEAM YAZIDI KUWA KUBWA.MASTAA WAONGEZEKA.



Ukiangalia katika picha hao ndio baadhi ya wasanii wanaomuunga mkono JIDE katika harakati za upingaji juu ya wanamziki kunyonywa katika kazi zao.
huyu mheshimiwa alijitoa kwa sababu amabazo alizitaja mwenyewe,sasa mashabiki wake inaonekana kumpinga vikali kwa huo uamuzi aliouchukua ikiwemo kupewa matusi na mashabiki wake.

MANENO YA ESMA DADA YAKE DIAMOND KUHUSU NDOA YAKE.



Esma Abdul ambae ni dada yake mwimbaji staa wa Tanzania, Diamond Platnums, amesema wamejiandaa vizuri kwa ajili ya harusi ya Diamond ambae anatarajiwa kumuoa mtangazaji wa TV aitwae Penny.

Esma ambae anaishi nyumba moja na kaka yake amesema, "Tumemkubali sana wifi yetu na tunampenda kwa sababu mtu yeyote mimi nitakaetambulishwa siwezi nikamkataa, manake nikimuingilia kwenye mapenzi yake na yeye ataniingilia kwenye mapenzi yangu."
Huu ni mwezi wa tano toka Esma amjue wifi yake ambae ni Penny, anasema nyumbani amekubalika na mipango ya harusi inaandaliwa japo hajui ni lini itafanyika, manake hiyo ni siri kwa sasa.

Zaidi ya wiki tano zilizopita, Diamond aliongea na kusema ndoa yake imekaribia kufungwa na huyo mkewe mtarajiwa ambae ni mjamzito lakini pia akathibitisha kumnunulia gari la kutembelea aliloliagiza nchini Japan - Hyundai IX 35.

Mpaka sasa Mwimbaji Diamond Platnums ambae aliongoza kwa kuwa msanii wa Tanzania alieandikwa sana kwenye internet 2012, ameshaingia kwenye headlines za kuwa mapenzini na mastaa wa kike Tanzania kipindi cha nyuma kama Jokate, Wema Sepetu na wengine.


Friday, May 17, 2013

WANAFUNZI WANAOJIUZA CBE NA UDSM MAJINA YAO HEWANI.

Wanafunzi wa kike wa chuo kikuu cha Dar es salaam [UDSM],Chuo cha elimu ya biashara [CBE]na chuo cha mamlaka ya Elimu na ufundi stadi [VETA],Dar es salaam ,wamefikishwa katika mahakama ya jiji samora wakidaiwa kufanya biashara ya kuuza mili yao. Washitakiwa hao waliokamatwa katika eneo la kona Baa Ambiance Sinza wilayani kinondoni ambao ni miongoni mwa wanawake 35 wanaodaiwa kufanya biashara hiyo na wote walifikishwa mahakamani hapo. Kesi hiyo ilikuwa chini ya hakimu Willian Mtaki ambapo muendesha mashitaka,bwana John Kijumbe,alisema wasichana hao walikamatwa katika mazingira tofautitofauti. Wanafunzi hao ni Yasinta Kilimo mwenye miaka 21 CBE mkazi wa upanga,Morin Masatu miaka 19 UDSM,mkazi wa kinondoni na mwanafunzi wa VETA aliyefahamika kwa jina moja la Khadija. “Nilikwenda pale baa kuchukua simu yangu ambayo ilipotea hivyo waliniita nikaichukue ndipo askari wa jiji wakanikamata,”Alisema Khadija akijitetea. Kwa mujibu wa bw. Kijumbe washitakiwa hao wamekosa dhamana baada ya kushindwa kutimiza masharti ya kila mmoja kuwa na wadhamini wawili au kulipa faini ya kulipa sh. 200,000. Kesi hiyo inatarajiwa kusikilizwa tena mei 28 mwaka huu,ambapo washitakiwa wote walipelekwa Segerea. Wakati huohuo, jeshi la Polisi mkoa wa kinondoni , limewakamata watuhumiwa 716 waliokuwa wakijihusisha na biashara ya kuuza miili kati yao wanaume 38 na wanawake 678. Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi mkoa wa kipolisi Kinondoni Charles Kenyela, alisema watu hao walikamatwa kwenye msako uliodumu kwa miezi sita kwenye maeneo mbalimbali ya Kinondoni. Maeneo hayo ni baa, kumbi za starehe, madanguro, sehemu za wazi katika ufukwe wa Bahari ya Hindi, na makaburini ambapo kati ya wanaume waliokamatwa wengine ni mashoga pamoja na wateja wa machagudoa. “Msako huo ulifanyika Maisha Club, Coco Beach, Barabara ya Tunisia , Travertine Hotel, Tandale Uwanja wa Fisi, Ambiance Club, Shekilango pamoja na Mwinanyamala” Alisema Kamanda Kenyela aliongeza kuwa , jeshi hilo pia limewakamata raia 12 kutoka nchini Ethiopia walioingia nchini bila kibali kati ya Mei 2 na 6, mwaka huu katika eneo la Kimara Mwisho na Tegeta Kibaoni. Alisema kukamatwa kwao kulitokana na taarifa walizozipata kutoka kwa raia wema waliowaona maeneo

T.I.D APOKEA MABANGO BAADA YA KUSUSA SHOO YA ANACONDA(LADY JAYDEE)


Wadau kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii wamemjia juu msanii mkongwe T.I.D ali maarufu kama mnyama.hiyo ni baada ya kususia shoo ya mwanadad JIDE inyotegemea kufanyika tarehe 31may.T.I.D anashutumiwa kufanya hicho kitu baada ya kushawishiwa na watu maarufu na wamiliki wa kituo kikubwa cha redio nchini.

Arafat.

arafat ngumi jiwe katika kashifa ya kuliwa kiboga baada ya kufamaniwa akimfanyia mtoto mambo hayo.

Mubaah Katela.

welcome to my blog.

LAMPARD SHUJAA WA MAGORI CHELSEA.

Mabao mawili ya Frank Lampard yaliifanya Chelsea kuibuka na ushindi wa 2-1 ugenini dhidi ya Aston Villa. Magoli hayo mawili aliyoyafunga Lampard ambaye ni nahodha msaidizi wa timu hiyo na timu ya taifa ya Uingereza, yamefanya avunje rekodi ya Bobby Tambling mchezaji wa zamani wa Chelsea na kuweka rekodi mpya ya kuwa mfungaji bora wa muda wote wa klabu hiyo ya mashariki mwa London baada ya kufikisha idadi ya kufunga jumla ya mabao 203 tangu aanze kuichezea The Blues. Chelsea walikuwa wageni kwenye uwanja wa Villa Park katika mechi ambayo ilikuwa na ushindani huku kadi mbili nyekundu zikitoka. Christian Benteke wa Aston Villa na Ramires wa Chelsea walipewa kadi nyekundu kwa nyakati tofauti. Kwa matokeo haya Chelsea sasa wanasalia kwenye nafasi ya tatu na pointi 72 huku Aston Villa wakiwa bado kwenye nafasi ya 13 na pointi 40. Michezo mingine ya ligi kuu ya England inayofikia tamati wiki ijayo itachezwa kwa nyakati tofauti hapo jumapili. Stoke City watakuwa wakipambana na Tottenham Hotspurs wakati Everton watakuwa nyumbani kuwakaribisha West Ham United. Kwingineko Fulham watawakaribisha Liverpool kwenye uwanja wa Craven Cottage huku Norwich wakitarajia kupapatauana na West Brom. Sunderland wao watakuwa wakicheza mchezo ambao kocha wao Paulo Di Canio ameuita mchezo wa fainali kwao dhidi ya Southampton,mchezo ambao utaamua hatima yao ya kushuka ama kusalia kwenye ligi kuu msimu ujao. Mabingwa Manchester United wao watacheza mchezo wao wa mwisho kwenye uwanja wa Old Trafford dhidi ya Swansea, mchezo ambao United watautumia kumuaga kocha wao Sir Alex Ferguson aliyetangaza kustaafu msimu ujao na pia watakuwa wakikabidhiwa rasmi kombe la ubingwa wa ligi kuu msimuu huu. Na mchezo wa mwisho QPR watakuwa wakipambana na Newcastle, mchezo ambao BBC Ulimwengu wa soka itakuwa ikutangazia moja kwa moja kuanzia majira ya saa kumi na moja na nusu jioni kwa saa za Afrika mashariki sawa na saa kumi na nusu Afrika ya kati.

VITA YASHIKA KASI NIGERIA.

Operesheni hiyo inakuja baada ya serikali kutangaza hali ya hatari katika majimbo ya Borno, Yobe na Adamawa Kaskazini Mashariki mwa nchi ambako watu 2,000 yatari wameuawa tangu mwaka 2009. Amri ya kutotoka nje kuanzia saa za jioni hadi asubuhi imetangazwa katika jimbo la Adamawa ili kukabiliana na wanamgambo hao. Mwandishi wa BBC katika jimbo la Adamawa anasema kuwa uamuzi huo unashangaza kwani hali ya usalama katika jimbo hilo sio mbaya ikilinganishwa na majimbo ya Borno na Yobe. Mnamo siku ya Alhamisi wanajeshi walivamia kambi za wanamgambo katika mbuga ya wanyama na ambayo inasifika kuwa moja ya ngome kuu za kundi la Boko Haram Msemaji wa jeshi la Nigeria Brigedia Generali Chris Olukolade, alisema kuwa watatumia uwezo wao wote wa kijeshi kukabiliana vilivyo na wapiganaji wa Boko Haram.

CD ZA UAMSHO MARUFUKU KUUZWA ZIPO NA ILUNGA.

Katika hali isiyo ya kawaida mjini Zanzibar cd za uamsho na zile za shekhe ILUNGA na mashehe wengine zimepigwa marufuku.Ni kwa kile kinachodaiwa kwamba CD hizo zinaleta uchochezi wa kidini ambao ni hatari kwa amani ya taifa na inasemakana ndo chanzo cha kulleta baina ya sintoelewana kati ya dini mbili waislamu na wakristo Nchini.

KUTOKA MTWARA.

Katika mji wa mtwara kulitegemewa leo kuwepo na maandamano ambapo mji huo umekumbwa na hofu kiasi kwamba baadhi ya biashara katika mji huo hazijafanyika.Mji huo umekuwa tulivu na polisi walionekana wakiranda randa katika mji huo.

MAGAZETI YA LEO IJUMAA TAREHE 17

MAGAZETI YA LEO IJUMAA TAREHE 17

KUTOKA MTWARA.

Katika mji wa mtwara kulitegemewa leo kuwepo na maandamano ambapo mji huo umekumbwa na hofu kiasi kwamba baadhi ya biashara katika mji huo hazijafanyika.Mji huo umekuwa tulivu na polisi walionekana wakiranda randa katika mji huo.