Hatimaye Barack Obama, Rais wa Marekani anatembelea tena bara la Afrika. Hii itakuwa ni mara ya pili Obama kutembelea Bara hili alikotoka baba yake baada ya ziara yake ya kwanza mwaka 2009. Mwaka huo alitembelea Ghana na Misri ilhali mwaka huu anatembelea Senegali, Afrika Kusini na Tanzania. Ziara hiyo itakayoanza tarehe 26 mwezi Juni, itamfikisha Tanzania tarehe 1 Julai na kuondoka siku ya pili yake.
Uchaguzi wa Obama kuwa Rais wa Marekani ulipokolewa kwa shangwe Afrika nzima. Wakati Waziri wa mambo ya nje wa Nigeria alilia kwa furaha, nchi ya Kenya ilitangaza siku ya mapumziko na Rais wa zamani wa Afrika Kusini ndugu Nelson ‘Madiba’ Mandela alisema ‘ushindi wa Obama unawafanya Waafrika wathubutu kuota ndoto (Jarida la The Economist). Hapa Tanzania kulikuwa kuna